Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:38:14
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Guterres ampongeza Donald J. Trump kwa kuchaguliwa Rais wa Marekani

    06/11/2024 Duración: 01min

    Kufuatia Donald J Trump kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Jumanne Novemba 5,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa salamu za pongezi. Taarifa iliyotolewa Jumatano asubuhi jijini New York, Marekani na msemaji wa Umoja wa Mataifa, imemnukuu Guterres akisema napongeza wananchi wa Marekani kwa ushiriki wao katika mchakato wa demokorasia.Kisha akasema nampongeza Rais Mteule Donald J. Trump na ninarejelea imani yangu kwamba ushirikiano kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa ni nguzo muhimu ya uhusiano wa kimataifa.Guterres amesema Umoja wa Mataiifa uko tayari kufanya kazi kwa kina na serikali ijayo ya Marekani il ikutatua changamoto kubwa zinazokabili dunia hivi sasa.Trump ambaye anawakilisha chama cha Repablikani, anakuwa Rais wa 47 wa Marekani.Amemshinda Makamu wa Rais Kamala Harris ambaye alikuwa anagombea kiti cha urais kupitia chama cha Demokrati.Hii ni mara ya pili Trump ataongoza Marekani kwani alikuwa Rais wa  45 wa Marekani kuanzia Januari 2

  • 06 NOVEMBA 2024

    06/11/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini Marekani, na watoto wanaotumikishwa jeshini na waasi nchini DRC. Makala tunakupeleka Havana nchini Cuba, na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kufuatia Donald J. Trump kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Jumanne Novemba 5, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa salamu za pongezi.Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC za kunasua watoto na vijana wanaotumikishwa vitani zinaendelea na tukio la hivi karibuni zaidi ni la kijana..Makala leo inatupeleka Havana Cuba ikiwa imesalia siku moja tu kabla ya kuanza kwa kongamano la kimataifa la Kiswahili lililobeba maudhui “Kiswahii  na teknolojia, na Kiswahili kama nyenzo ya kudumisha  amani na maendeleo”.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kwa mwanamke mwandishi wa habari akitueleza jinsi wanavyochochea haki za binadamu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

  • Simulizi ya Ombeni baada ya kutoroka waasi na kurejea uraiani huko DRC

    06/11/2024 Duración: 02min

    Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC za kunasua watoto na vijana wanaotumikishwa vitani zinaendelea na tukio la hivi karibuni zaidi ni la kijana.Katika video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ombeni anasimulia jinsi waasi wa FDLR mashariki mwa DRC walivyowakamata msituni."Tulikuwa vijana watanoFDLR walitukamata na kutupeleka msituni. Maisha ilikuwa ngumu sana na hatukuweza kutoroka"Kazi wanatumikishwa bila mshahara na zaidi ya yote."Kila saa ni mateso, kazi mingi bila malipo."Alitumikishwa msituni kwa miaka minane, akionesha makovu ya vipigo alivyopatiwa."Tuliteseka sana, tulitumikishwa kwa muda wa miaka minane, tukachapwa viboko, tuliumizwa sana na kubaki na majeraha"Lakini siku moj aliweza kutoroka. Akiwa Kibirizi akamweleza mkubwa wake ya kwamba.." Siku moja nikamwambia mkubwa wangu naenda kusalamia rafiki yangu, wakati huo tukapata nafasi ya kutoroka."Katika harakati hizo akakutana na MONUSCO. Anasema kwam

  • 05 NOVEMBA 2024

    05/11/2024 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia uvuvi katika mji wa Kalokol karibu na fuo za Ziwa Turkana Kaskazini mwa Kenya. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkutano wa WUF12 Cairo Misri, chanjo ya malaria Sudan, siku ya Tsunami, na mashinani.Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Miji Duniani, WUF12 umeingia siku ya pili hii leo huko Cairo, Misri, ambako Ming Zing ambaye ni Mkurugenzi wa Miji, Mnepo na Ardhi kutoka Benki ya Dunia amezungumzia umuhimu wa kujumuisha wanawake na vijana katika mipango miji.Sudan imekuwa nchi ya 16 barani Afrika na ya kwanza katika Ukanda wa WHO wa Mashariki na Mediterania kuanzisha chanjo dhidi ya Malaria kwa watoto wasiozidi umri wa miezi 12. Chanjo imeanza kutolewa jana katika majimbo ya Gedaref na Blue Nile ambapo WHO na wadau wamesema mwaka 2025 na 2026 chanjo itapelekwa katika maeneo 129 nchini kote Sudan.Na leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu tsunami, ambayo ni mawimbi makubwa ya maji yatokanayo na tetemeko chini ya bahari. Katibu Mkuu wa Umoja

  • Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wasaidia watoto yatima huko Beni, DRC

    04/11/2024 Duración: 03min

    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mapigano kati ya jeshi la serikali, FARDC na vikundi vilivyojihami, yamesababisha vifo na hata watu kufurushwa makwao. Watoto wamesalia yatima na hawana walezi. Vituo vya kulea watoto yatima vimebeba jukumu la kuwatunza, lakini navyo viko taabani. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa, kutoka Tanzania, TANZBATT-11 wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO waliguswa na kuamua kujiongeza na kuwasilisha msaada kwa watoto hao. Afisa Habari wa TANZBATT-11 Kapteni Fadhillah Nayopa anasimulia kile walichofanya.

  • UN: Baada ya janga la njaa, sasa kipindupindu na homa ya kidingapopo yaikumba Sudan

    04/11/2024 Duración: 01min

    Nchini Sudan ambako vita na njanga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia  sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa  la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani. Asante Assumpta kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA na lile la afya duniani WHO, hali inazidi kuwa mbaya Sudan ambako katikati ya vita majanga mingine ya kiafya yanazuka.OCHA imeripoti zaidi ya wagonjwa 28,000 wa kipindupindu na vifo vimefikia 836 katika majimbo 11 kati ya 22 Julai na 28 Oktoba mwaka huu huku likihofia kwamba idadi kamili ya wagonjwa huenda ni kubwa zaidi.Pia shirika hilo limeonya juu ya kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa homa ya kidingapopo na mvua zinazonyesha na kusababisha mafuriko makubwa zimeongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa hayo.Nalo shirika la WHO linasema milipuko hii imezuka

  • 04 NOVEMBA 2024

    04/11/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Sudan unaosababisha janga la njaa, na mradi wa maji Galmudug Somalia kwa ajili ya maji safi na salama pamoja na mifugo. Makala tunakupeleka nchini DR Congo na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Nchini Sudan ambako vita na janga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia      sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa  la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani.Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika.Makala inakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako Kapteni Fadhillah Nayopa, Afisa habari wa kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania, TANZBATT-11 katika ujumbe wa Umoja wa Matai

  • UNICEF na wadau Somalia wafanikisha mradi wa maji kwa wakazi wa Galmudug

    04/11/2024 Duración: 02min

    Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika. Tuko Adale, mji wa ndani zaidi wa jimbo la kati mwa Somalia, Galmudug. Hapa zaidi ya kaya 2,000 sasa zina huduma ya maji safi na salama, kufuatia ukarabati wa kisima cha maji.Salada Mohammed Omar, yeye ni mfugaji na ni shuhuda wa mradi huu uliotekelezwa na serikali ya jimbo la Galmudug kwa ufadhili wa shirika la Marekani la Misaada ya kimaendeleo USAID na UNICEF.“Tulisafiri muda mrefu kuteka maji, lakini sasa kisima kiko karibu na makazi yetu, tunapata kwa urahisi maji ya kupikia, kufulia na kufanyia usafi.”Video ya UNICEF inaonesha raia na ngamia wakiwa kisimani. Mohammed Yusuf Dirshe ambaye ni kiongozi wa kijamii hapa Adale anasema “awali hakukuwa na tanki la maji wala pampu. Kwa hiyo ilikuwa vigumu kupata

  • Asante WFP kwa msaada wa pesa taslim uliotuwezesha kiuchumi - Esther Josephine

    01/11/2024 Duración: 03min

    Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Chakula Duniani WFP,  ungali unaendelea kuwasaidia wakimbizi wa ndani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kurejesha tabasamu la waliopoteza makazi yao kutokana na hali ya ukosefu wa usalama nchini humo. Chakula na pesa taslimu zilitolewa kwa wale wanaohitaji jimboni Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC. Mwandishi wetu George Musubao amekutana na Esther Josephine, mama wa watoto 3 aliyekimbia kutoka Kitsanga kwa sababu ya mapigano kati ya jeshi la serekali ya DRC (FARDC) na waasi wa M23, na anatueleza jinsi mama huyu amewezakujikwamua kiuchumi katika makala hii.

  • UNICEF Kenya wafanikisha mapambano dhidi ya kipundupindu Lamu

    01/11/2024 Duración: 02min

    Serikali ya Kaunti ya Lamu katika pwani ya kaskazini ya Kenya, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanaendesha shughuli ya kuwafikia wanajamii ili kubadilishana taarifa kuhusu jinsi watu wanaweza kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kutoa huduma za maji, vifaa vya kujisafi na usafi kwa jamii zilizoathirika. Kutoka katika video iliyoandaliwa na UNICEF.Wamekaa chini ya mti, wanawake kwa wanaume. Nyuma ni nyumba ya makuti na matumbawe, Lamu, Pwani ya Kenya. Muelimishaji wa masuala ya afya anawaeleza namna ya kuweka mazingira safi ili kupambana na kipindupindu. Mwanajuma Kahidi yamewahi kumkuta. Anaposema Cholera anamaanisha hiyo hiyo kipindupindu iliyokuwa imetishia Uhai wake na familia yake.“Nilipopata maambukizi ya Kipindupindu nilihisi siko sawa kwa sababu nilikosa nguvu na nikakosa raha na nikapoteza nuru ya macho ndio nikakimbilia hospitali. Huo ugonjwa ulipitia kwenye maji na chakula. Mimi na watoto wangu tulipatwa na kipind

  • 01 NOVEMBA 2024

    01/11/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko katika ukanda wa Gaza na masuala ya afya nchini Kenya. Makala inatupeleka nchini DRC kumsikia mkimbizi mjasiriamali na mnufaika wa pesa taslimu kutoka WFP, na mashinani tunakupeleka nchini Lebanonon kwa waathirika wa vita.Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza inazidi kuzorota huku raia na hata wafanyakazi wa kutoa misaada wakisalia wamepigwa butwaa kwani mashambulizi kutoka Israeli yanaendelea kila uchao.Serikali ya Kaunti ya Lamu katika pwani ya kaskazini ya Kenya, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanaendesha shughuli ya kuwafikia wanajamii ili kubadilishana taarifa kuhusu jinsi watu wanaweza kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kutoa huduma za maji, vifaa vya kujisafi na usafi kwa jamii zilizoathirika. Kutoka katika video iliyoandaliwa na UNICEF.Makala George Musubao, mwandishi wetu wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DR

  • Raia na hata wahudumu wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza wamekata tamaa

    01/11/2024 Duración: 01min

    Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza inazidi kuzorota huku raia na hata wafanyakazi wa kutoa misaada wakisalia wamepigwa butwaa kwani mashambulizi kutoka Israeli yanaendelea kila uchao. Naanzia ndani ya hospitali ya Kamal Adwan  kaskazini mwa Gaza, mtoto aliyejeruhiwa amebebwa akilia kwa uchungu. Kwingineko mgonjwa mwingine anatolewa kwenye gari la wagonjwa! Ni taswira iliyozoeleka sasa Gaza.Louise Wateridge ambaye ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Dharura katika shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kutoka Gaza Kati amesema hali si hali.Anasema, “mambo kwa kweli yanazidi kuwa mabaya hapa. Kukata tamaa ni kila mahali. Namaanisha, watu unaozungumza nao, na wafanyakazi wenzangu niliozungumza nao hawajui sasa wafanye nini. Hawafahamu waende wapi. Unaweza kusikia nyuma yangu milio ya makombora ikiendelea.”Bi. Wateridge akaendelea kusema kuwa, “kutokuwa na matumaini ndio neno

  • ZMBF na harakati zao za kukabili udumavu Zanzibar

    31/10/2024 Duración: 05min

    Zanzibar Maisha Bora Foundation iliyoko Tanzania Zanzibar, iliyoanzishwa mwaka 2021 tayari inajinasibu na harakati za kusongesha afya ya watoto halikadhalika kupinga udhalilishaji wa kijinsia, masuala ambayo Umoja wa Mataifa kila uchao unasaka wadau wa kuunga mkono ili dunia pawe pahala salama kwa kila mtu na kila mtu aweze kustawi. Ni kwa kutambua hilo, Assumpta Massoi wa Idhaa hii alipopata fursa ya kuzungumza na Muasisi na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Bi. Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mke wa Rais wa Zanzibar, wakati wa ziara yake hapa Umoja wa Mataifa hivi karibuni aliona vema Bi. Mwinyi atufafanulie kwa kina wanachofanya, na alianza na kwa kueleza sababu ya kumulika lishe bora kwa watoto Zanzibar.

  • Jifunze Kiswahili - Ufafanuzi wa neno HEREREZA na Dkt. Mwanahija Ali Juma

    31/10/2024 Duración: 37s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEREREZA! 

  • 31 OKTOBA 2024

    31/10/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina mada kwa kina inayotupeleka Zanzibar nchini Tanzania kupata ufafanuzi wa jukumu la “Zanzibar Maisha Bora Foundation” akitueleza Bi. Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mke wa Rais wa Zanzibar, wakati wa ziara yake hapa Umoja wa Mataifa hivi karibuni. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno HEREREZA.Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo na mashirika yake lile la mpango wa chakula (WFP) na la chakula na kilimo (FAO), uhaba mkubwa wa chakula unatarajiwa kuongezeka kwa ukubwa na ukali katika nchi na maeneo 22 duniani. Ripoti hiyo inaonya kwamba kuenea kwa migogoro, hasa katika Mashariki ya Kati inasukuma mamilioni ya watu ukingoni.Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, amelaani vikali shambulio la jana usiku lililotekelezwa na Jeshi la Urusi ambapo jengo la makazi la ghorofa nyingi lilipigwa katika mji wa Kharkiv, wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya majiji,

  • Fahamu kuhusu mtikisiko wa ubongo

    30/10/2024 Duración: 01min
  • UNRWA yamwandikia Rais wa Baraza Kuu la UN baada ya Knesset kupitisha miswada

    30/10/2024 Duración: 01min
  • 30 OKTOBA 2024

    30/10/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akimulika masuala ya amani na usalama hususan Gaza; afya ya ubongo kwa wanamichezo; biashara ya ndizi kaukau huko India na dansi na kujitambua huko Trinidad na Tobago.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina,  UNRWA, Philippe Lazzarini amemwandikia barua Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kusaka mshikamano na nchi wanachama baada ya Bunge la Israeli Jumatatu hii kupitisha miswada ya kusitisha shughuli za shirika hilo.  Flora Nducha na maelezo zaidi.. Hoja ya ubongo kutikisika (concussion) wakati wa michezo imeibuka katika siku za karibuni na kulazimu Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) kuingilia kati ili kudadavua kwa kina. Akiwa uwanjani akitazama mpira wa Daktari Tarun Dua, Mkuu wa Kitengo cha Afya ya Ubongo WHO, anaeleza kwa muhtasari kuhusu tatizo hilo kupitia taarifa ya Cecily Kariuki.Katika makala, Assumpta Massoi anakupeleka barani Asia, kusikia jinsi wazo la biashara kuto

  • Mwelekeo ni kutengeneza kaukau za ndizi zenye ladha ya kitunguu na nazi

    30/10/2024 Duración: 03min

    Uwekezaji rahisi kabisa kwa familia ya Didiki huko nchini India umekuwa na manufaa kwa kaya zaidi ya 20. Zao la ndizi ambalo awali hawakuweza kuongeza thamani ipasavyo lilikuwa na manufaa kidogo kiuchumi. Somo la biashara likamfungua fikra Didiki hadi kupata msaada kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo IFAD kwa ushirikiano na serikali ya India. Msaada umepanua biashara, vijana wamepata ajira, familia zimeongeza kipato na sasa mpango ni kufikia kaya zaidi ya 60,000. Ni kwa vipi? Ungan ana Assumpta Massoi kwenye makala hii.

  • 29 OKTOBA 2024

    29/10/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kuwasikia vijna ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu UNRWA, na Siku ya kimataifa ya huduma, na mashinani.Baada ya Bunge la Israel hapo jana Oktoba 28 kupiga kura ya kuizuia Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kufanya shughuli zake katika maeneo yote yaliyoko chini ya Israel, viongozi wa Umoja wa Mataifa kuanzia Katibu Mkuu Antonio Guterres wameendelea kupaza sauti kwamba kuizuia UNRWA ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa na italeta zahma kwa maisha ya watu katika eneo hilo la Mashariki ya Kati. Katibu Mkuu Guterres amesema analileta suala hili kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na atahakikisha Baraza hilo muda wote linakuwa na taarifa kwa kadri hali inavyoendelea.Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa  wa kutafuta ukweli nchini Sudan

página 2 de 5