Habari Za Un

Balozi Lokaale: Licha ya changamoto  hakuna taasisi mbadala wa UN duniani

Informações:

Sinopsis

Ilikuwa miezi, wiki na sasa imesalia siku tatu tu kabla ya mjada mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 kun’goa nanga hapa kwenye Makao Makuu jijini New York Marekani ambapo viongozi wa Dunia na wakilishi mbalimbali watashiriki kwenye mkutano wa 80 wa Baraza Kuu. Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa. Flora Nducha ameketi na mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ekitela Lokaale kuzungumzia Afrika na Umoja wa Mataifa katika miaka na umuhimu wa Umoja huo duniani, hiki ni kionjo tu cha maohojiano hayo akianza na mchango wa Afrika Umoja wa Mataifa