Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:54:46
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • 25 FEBRUARI 2025

    25/02/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC ambako ghasia za hivi karibuni huko Goma zimeongeza mahitaji ya huduma za afya, WHO imechangia vifaa muhimu vya matibabu ili kukabialiana na hali hiyo. Pata pia muhtasari wa habari na mashinani.Kufuatia ripoti za kuweko kwa ugonjwa usiojulikana huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao tayari umeambukiza mamia ya watu na kusababisha makumi ya vifo, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, limesema bado linaendelea na uchunguzi wa ugonjwa huo uliotangazwa kwa chapisho la kikanda la WHO.Kampeni ya chanjo ya polio inayoendelea ukanda wa Gaza kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya polio na kuzuia tishio la ugonjwa huo kusambaa maeneo mengine na nchi jirani, imekuwa na mafanikio makubwa kwani hata eneo la Gaza Kaskazini, mwitikio ulikuwa mkubwa licha ya mvua na baridi kali.Na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo limetangaza kuwa sitisho la mapigano Gaza limewezesha kufikisha eneo hilo kwa wa

  • Gaza: Awamu ya tatu ya chanjo dhidi ya polio inaendelea

    24/02/2025 Duración: 03min

    Katika makala hii Anold Kayanda wa Idhaa hii anaangazia chanjo inayoendelea katika Ukanda wa Gaza dhidi ya polio chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya ya Palestina kwa kusaidiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa. Uchanjaji huu wa sasa kwa njia ya matone dhidi ya polio ni wa dharura kutokana na kugunduliwa kwa virusi vya polio katika sampuli za maji taka huko Gaza hivi karibuni, ikionesha kuwa virusi hivyo vinaendelea kuzunguka katika mazingira na hivyo kuwaweka watoto katika hatari. 

  • UNICEF na WFP wawezesha watoto nchini Sudan Kusini kwenda shule ili watimize ndoto zao

    24/02/2025 Duración: 02min

    Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Kuhudumia Watoto, UNICEF na la Mpango wa Chakula duniani, WFP kwa kushirikiana na mradi wa pamoja wa kimataifa wa mnepo ,au Joint Resilience Project (JRP) nchini Sudan Kusini ,wanatekeleza msaada wa chakula bora na salama bila malipo kwa watoto shuleni ,kwa zaidi ya wanufaika laki tano alfu Hamsini 550,000 ili kuhakikisha ndoto za watoto hao zinatimia. Ni sauti ya watoto wakitembea kuelekea shuleni huku wakiwa wamevibeba vitabu vyao mikononi.Kupitia video iliyoandaliwa na UNICEF, Tieng Maleng, mnufaika wa mradi wa JRP kutoka kijiji cha Pangapdit anaonekana akiwapa watoto wake kiamsha kinywa huku wakiwa wamekaa nje ya boma lao wakiwa wamevalia sare zao tayari kwenda shule. Kwa furaha anaeleza jinsi mradi huu umekuwa wa manufaa kwa familia yake.“Baada ya kupokea msaada wa kifedha, nilitumia fedha kidogo kulipa ada ya shule ya watoto wangu. Nikachukua sehemu kidogo ya fedha hizo kununua viatu vyao, na dawa. Pia nilitumia sehemu nyingine ya msaada huo katika kilimo

  • 24 FEBRUARI 2025

    24/02/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia miaka mitatu ya vita nchini Ukraine, machafuko nchini DRC na elimu Sudan Kusini. Makala inatupeleka katika ukanda wa Gaza kumulika harakati za chanjo ya polio, na mashinani nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mama.Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano  yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia

  • Ukraine: Miaka 3 ya kumbukumbu mbaya, juhudi zifanyike mzozo uishe - Guterres

    24/02/2025 Duración: 02min

    Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano  yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu. Selina Jerobon na taarifa kamili..

  • Hofu ya raia zaidi kukimbia DRC kuelekea Burundi, UNHCR yasaka dola milioni 40.4 za kuwasaidia

    21/02/2025 Duración: 02min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa ombi la dola milioni 40.4 ili kujiandaa na kutoa huduma za kuokoa maisha na usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na waliokimbilia nchi jirani baada ya wakati huu ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yanazidi kufurusha raia kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • Maelfu wavuka mto Rusizi kwa mtumbwi kutoka DRC na kuingia Burundi ili kuokoa maisha yao

    21/02/2025 Duración: 05min

    Maelfu ya watu wanawasili nchini Burundi, wakikimbia mapigano yanayozidi kushamiri huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini. Waasi wa M23 wanaendelea kupanua wigo wa maeneo wanayomiliki, hali inayotumbukiza raia kwenye changamoto za usalama, na kulazimu wale wanaoweza kukimbia. Wengine wameuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, na majeruhi wako hospitalini ambako huduma nazo zimedorora kwani M23 wamefunga barabara katika maeneo yote wanayodhibiti. Lakini wale wanaokimbilia Burundi hali yao iko vipi? Evarist Mapesa anakusimulia zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

  • 21 FEBRUARI 2025

    21/02/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia mahitaji ya wakimbizi wanaokimbia machafuko DRC wakielekea nchini Burundi, na hali ya wakimbizi wa ndani Gaza wakati huu wa msimu wa baridi. Makala tunakurejesha nchini DRC na mashinani tunakwenda nchini Tanzania.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa ombi la dola milioni 40.4 ili kujiandaa na kutoa huduma za kuokoa maisha na usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na waliokimbilia nchi jirani baada ya wakati huu ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yanazidi kufurusha raia kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.Katika makala Evarist Map

  • Watoto watota kwa mvua katika ukanda Gaza, huku baridi kali ikitishia afya zao

    21/02/2025 Duración: 02min

    Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya. Ni sauti ya watoto wakitembea katikati ya mahema ya muda kwenye vichochoro vilivvyojubikwa na matope, hapa Gaza Kaskazini, huku wakijaribu kukwepa madimbwi ya maji yaliyosababishwa na mvua kubwa.Kupitia video iliyoandaliwa na UNICEF, Shahd Omar, msichana mwenye umri wa miaka kumi na saba, anaonekana amembeba nduguye, wengine wanaonekana wamekujikunyata kutokana na baridi. Shahd sasa akiwa amesimama nje hema lao anaelezea jinsi nyumba zao zilivyoharibiwa.“Tunavumilia hali ngumu sana,mvua kubwa, baridi, na upepo mkali, maisha ni magumu sana. Nyumba yetu ilivyoshambuliwa na kubomoka tulijitoa kwenye vif

  • Jifunze Kiswahili: Upatanisho wa kisarufi wa baadhi ya maneno

    20/02/2025 Duración: 52s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Mlumbi wa Lugha Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua upatanisho wa kisarufi wa baadhi ya maneno kama vile "Ng'ombe kumi na minane ", vikombe viwili na mengineyo ambayo watu hutamka vibaya katika sentensi, mfano "Ng'ombe kumi na nane"

  • 20 FEBRUARI 2025

    20/02/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani mada kwa kina ikimulika harakati za uhamasishaji kabla na baada ya maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani iliyoadhimishwa hivi karibuni na mchango wa redio katika juhudi za uhifadhi wa mazingira na kuchagiza maendeleo ya jamii huko Ramogi nchini DRC. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa maneno.Idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walioingia Burundi kufuatia mashambulizi yanayofanywa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, mashariki mwa DRC sasa imeongezeka na kufikia 20,000.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, limechapicha picha zikionesha wakimbizi walio njiani wakipikiwa chakula, wakati huu ambapo M23 wametwaa miji ya Goma jimboni  Kivu Kaskazini, na Bukavu na Kamanyola jimboni Kivu Kusini.Na katika hatua nyingine ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ikipatiwa jina UNJHRO imeripoti jinsi kutoroka kwa wafungw

  • Tanzania yataja mambo ya kuzingatiwa ili ulinzi wa amani uwe na tija

    19/02/2025 Duración: 03min

    Historia ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ulianza miaka mitatu tu baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa wenyewe. Na kutokana na umuhimu wa ulinzi wa amani kote duniani, shughuli hiyo imedumu kwa miaka yote hiyo 77 hadi sasa na bado ni muhimu lakini inaendelea kukumbwa na changamoto kama anavyofafanua Brigedia George Mwita Itang’are wa Tanzania, moja ya nchi 10 duniani zinazochangia zaidi vikosi vya ulinzi wa amani.

  • OCHA yasihi kufunguliwa kwa viwanja vya ndege Goma na Kavumu - DRC

    19/02/2025 Duración: 01min

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

  • 19 FEBRUARI 2025

    19/02/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini DRC, na simulizi y amkimbizi wa DRC aliyekimbilia nchini Uganda. Makala inatupeleka nchini Tanzania, namashinani nchini Kenya, kulikoni?Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia.Sina mpango tena wa kurejea nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni kauli yake Twagirayesu Gato, mwanafunzi huyu raia wa DRC aliyekimbia  nchini mwake mwaka jana na kuingia Uganda ambako sasa anapata hifadhi. Amesema hayo kwenye video ya shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyochapishwa katika ukurasa wa YouTube wa shirika hilo.Makala inatupeleka nchini Tanzania ambako tunamsikiliza Brigedia Jenerali George Mwita Itang’ar

  • Mkimbizi kutoka DRC aliyekimbilia Uganda akumbuka ukatili uliofanywa na waasi

    19/02/2025 Duración: 02min

    Sina mpango tena wa kurejea nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni kauli yake Twagirayesu Gato, mwanafunzi huyu raia wa DRC aliyekimbia  nchini mwake mwaka jana na kuingia Uganda ambako sasa anapata hifadhi. Amesema hayo kwenye video ya shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyochapishwa katika ukurasa wa YouTube wa shirika hilo. Kufahamu msingi wa kauli hiyo ya Twagirayesu, ungana na Sharon Jebiichi.

  • 18 FEBRUARI 2025

    18/02/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo inayotupeleka DRC katika mji wa Goma uliokuwa mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini ambao sasa uko mikoni mwa waasi wa kundi la M23. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ujumbe kutoka mashinani.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR imesema hali huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC inazorota kwa kasi kubwa, na kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ukatili kama vile watu kuuawa kiholela, wakiwemo watoto, wakati huu ambapo waasi wa M23 yaripotiwa wametwaa mji wa Bukavu, jimboni Kivu Kusini.Wakati hayo ya kiendelea ndani ya DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeripoti kuwa katika siku chache zilizopita, wakongo kati ya 10,000 na 15,000 wamevuka mpaka wa DRC na kuingia Burundi wakikimbia mapigano.Na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP limekaribisha mchango wa dola milioni 5 kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini. kwa ajili ya kujengea mnepo na kuimarisha upatika

  • Mradi wa ufugaji bora wa mbuzi umenikwamua – Mfugaji Kigoma

    17/02/2025 Duración: 04min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini Tanzania linaendelea kutekeleza Programu ya pamoja kwa mkoa wa Kigoma KJP iliyoanza kutekelezwa nchini humo mwaka 2017 na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto za kipekee za mkoa huo ikiwemo zitokanazo na kuhifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani.Miongoni mwa miradi inayotekeleza ni ule wa kupatia wananchi mafunzo ya ufugaji bora wa mbuzi ili waweze kuinua kipato chao na vile kuimarisha lishe kwenye familia.Kupitia video ya FAO, utamsikia mnufaika wa mafunzo hayo kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.

  • Dola bilioni 6 zahitajika kusaidia kukabiliana na janga la kibinadamu nchini Sudan

    17/02/2025 Duración: 01min

    Kutokana na hali tete ya kibinadamu nchini Sudan, Umoja wa Mataifa na wadau wake leo Februari 17 jijini Genea, Uswisi, wamezindua mipango ya misaada ya kibinadamu na wakimbizi kwa mwaka huu 2025 kwa Sudan, wakihitaji jumla ya dola bilioni 6 kusaidia karibu watu milioni 26 ndani ya Sudan na kanda nzima.  Selina Jerobon na maelezo zaidi.

  • 17 FEBRUARI 2025

    17/02/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu kwa wakimbizi na raia wa Sudan, na maradi wa lishe bora kwa watotot nchini Kenya. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Zambia, kulikoni?Kutokana na hali tete ya kibinadamu nchini Sudan, Umoja wa Mataifa na wadau wake leo Februari 17 jijini Genea, Uswisi, wamezindua mipango ya misaada ya kibinadamu na wakimbizi kwa mwaka huu 2025 kwa Sudan, wakihitaji jumla ya dola bilioni 6 kusaidia karibu watu milioni 26 ndani ya Sudan na kanda nzima.Mradi unaoendeshwa na serikali ya kenya  na kupigwa jeki na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambao ni wa kuboresha lishe kwa watoto kwa kugawa fedha taslim na elimu ya afya au NICHE (NISHI) umeleta nuru kwa wakazi wa Lokichar katika kaunti ya Turkana Kaskazini Mashariki mwa Kenya na miongoni mwa wanufaika ni Leah Akiru.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini Tanzania anakuletea mnufaika wa mafunzo ya ufugaji bora wa mbuz

  • Mradi wa NICHE umekuwa mkombozi wangu, asante UNICEF: Leah Akiru

    17/02/2025 Duración: 02min

    Mradi unaoendeshwa na serikali ya kenya  na kupigwa jeki na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambao ni wa kuboresha lishe kwa watoto kwa kugawa fedha taslim na elimu ya afya au NICHE (NISHI) umeleta nuru kwa wakazi wa Lokichar katika kaunti ya Turkana Kaskazini Mashariki mwa Kenya na miongoni mwa wanufaika ni Leah Akiru. Ungana na Flora Nducha kwa taarifa zaidi

página 5 de 5