Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:54:46
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • 06 MACHI 2025

    06/03/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Umoja wa Mataifa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP nchini Tanzania, unaolenga kuhakikisha wanawake na wasichana wanajumuishwa kwenye mipango ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kwa kuwajengea uwezo.Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, tathmini mpya ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo ikiangazia haki za wanawake miaka 30 baada ya Azimio la Beijing inaonesha uwepo wa maendeleo katika usawa wa kijinsia, kama vile sheria dhidi ya ubaguzi na sera jumuishi za kijinsia. Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza uwepo bado wa ubaguzi wa kijinsia uliojikita katika jamii, ukiendelea kuwazuia wanawake na wasichana kupata fursa.Ripoti nyingine ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo ikiangazia Sudan imefichua vitendo vya watu kukamatwa kiholela, mateso, na unyanyasaji huko Khartoum vinavyotekelezwa na Vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) na pia Jeshi la Serikali ya Sudan (SAF). Ripoti hiyo imearifu pia kuwa m

  • Hali ya usalama ikidorora DRC, hofu sasa ni mustakabali wa watetezi wa haki za binadamu

    05/03/2025 Duración: 01min

    Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi. (Taarifa ya Anold Kayanda)Mary Lawlor akizungumza leo jijini Geneva-Uswisi amesema, "watetezi wa haki za binadamu mashariki mwa DRC wako hatarini sana kulengwa na kulipiziwa kisasi kwa kazi yao ya kutetea haki za binadamu. Wanahitaji msaada sasa, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa kuhamishwa kwa muda pamoja na familia zao.”Kundi la waasi la M23, limeendelea kusonga mbele katika eneo hilo la mashariki mwa DRC tangu lilipoanza mashambulizi yake mapema mwaka huu, na wale waliorekodi na kufichua ukiukwaji wa haki zao wamekuwa wakilengwa moja kwa moja, amesisitiza Bi. Lawlor."Katika wiki za hivi karibuni nimepokea taarifa nyingi za tahadhari zinazohitaji msaada na nimezungumza moja kwa moja

  • Miaka 30 baada ya Azimio la Beijing kuhusu haki za wanawake, safari bado ni ndefu

    05/03/2025 Duración: 02min

    Kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa  shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawake hazipaswi tu kukumbukwa bali zinahitaji kutekelezwa kikamilifu. Flora Nducha anafafanua zaidiAkizungumza wiki hii mjini Geneva Uswisi katika majadiliano ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Beijing (#Beijing30), Bi. Bahous amebainisha umuhimu wa kuharakisha maendeleo ya usawa wa kijinsia akiwataka viongozi wa dunia kuchukua hatua thabiti ili kuhakikisha haki za wanawake zinapewa kipaumbele wakati wa changamoto zinazoendelea duniani.Amesema “Miaka 30 iliyopita dunia iliweka ahadi ya kusongesha fursa na utu wa wanawake na wasichana wote. Ahadi hiyo haikuwa maneno matupu kwenye karatasi, ilikuwa ramani ya njia na wito wa mshikamano . Na kwa

  • 05 MACHI 2025

    05/03/2025 Duración: 09min

    Hii leo jarida linamulika wasiwasi kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu nchini DRC, wakati huu hali ya usalama si shwari mashariki mwa nchi; kuelekea siku ya wanawake duniani, Mkuu wa UN Women arejelea Azimio la Beijing; vilabu vya Dimitra  nchini DRC vinavyosaidia wanawake na wanaume kuketi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabilia; mashinani ni Ramadhani huko Gaza.Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa  shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawak

  • Vilabu vya Dimitra vyaimarisha usawa wa kijinsia na uchumi DRC

    05/03/2025 Duración: 04min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limesaidia kujenga utangamano wa kijamii kwa kuboresha maisha kwenye eneo la Walungu jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Limefanya hivyo kupitia vilabu vya Dimitra ambavyo hupatia wanawake, wanaume na vijana fursa ya uongozi wa kuleta mabadiliko chanya kwa kutatua changamoto zilizo kwenye jamii yao bila hata kuwa tegemezi kwa msaada wa nje. Mradi huu ulitekelezwa kati ya mwaka 2008 na 2023 na sasa tunamulika ni kwa vipi umeleta mafanikio. Sharon Jebichii anaelezea kwenye makala hii kupitia video iliyoandaliwa na FAO. 

  • 04 MACHI 2025

    04/03/2025 Duración: 10min

    Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania (TPTC) kilichoko chini ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ/TPDF) kinavyotumia  sanaa ya muziki kuelimisha walinda amani kuhusu ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kingono. Makala hii iliyokusanywa na Florean Kiiza wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kwa kushirikiana na Kapteni Mwijage Francis Inyoma wa JWTZ imechakatwa na Anold Kayanda na inasimuliwa na Flora Nducha.

  • Napenda sana maabara na imenihamasisha kusoma sayansi - Zamzam

    03/03/2025 Duración: 02min

    Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Baadhi ya wasichana wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya ni wanufaika wa mpango huu. Sharon Jebiichi na maelezo zaidi.Zamzam Hussein,aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Hagadera. Ni mkimbizi mwenye asili ya Somalia na sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya akiwa na ndoto ya kuwa daktari. Kupitia mpango huu ambao ni sehemu ya programu ya PROSPECTS ambao ni ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao Zamzam Hussein ameweza kukumbatia sayansi.“Nilikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Hagadera na nikamaliza elimu yangu mwaka wa 2024. Nilijiunga na shule hiyo Agosti 2021

  • Viongozi wababe, wa kiimla na wenye fedha wanasigina haki za binadamu duniani

    03/03/2025 Duración: 02min

    Kwenye kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendellea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa M ataifa, Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani kote akielezea wasiwasi mkubwa kuhusu kudhoofika kwa makubaliano ya kimataifa kuhusu haki za binadamu,na kuonya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Anold Kakayanda na taarifa kamili.Asante Flora katika taarifa yake Türk  amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi haki za binadamu na utawala wa sheria ili kuzuia kurudiwa kwa ukatili wa zamani.Moja ya masuala ya dharura yaliyotiliwa mkazo na Türk  ni mgogoro wa kibinadamu unhaoendelea huko Gaza. Amelaani uharibifu uliosababishwa na hatua za kijeshi za Israeli dhidi ya mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina.Türk  amesisitiza haja ya kudumisha usit

  • Burundi yahamishia wakimbizi wa DRC eneo salama zaidi

    03/03/2025 Duración: 03min

    Machafuko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) yanaendelea kufurusha watu na wengine wanaamua kukimbilia nchi jirani ikiwemo Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Burundi limesema wazi kuwa katika wiki mbili za mwezi Februari kuanzia tarehe 14 walipokea wakimbizi zaidi ya 60,000, wengi wakiwa tayari walishafurushwa awali. Kwa waliowasili katika eneo la Kaburantwa  nchini Burundi, bado wanahofia usalama. Serikali ya Burundi imetenga eneo lingine salama zaidi na sasa wanahamishiwa huko. Je ni wapi? Assumpta Massoi kwa msaada wa video ya UNHCR Burundi anasimulia zaidi. 

  • 03 MACHI 2025

    03/03/2025 Duración: 11min

    Karibu jaridani hii leo na mwenyeji wako ni Flora Nducha akikuletea habari kuhusu haki za binadamu, elimu ya STEM kwa wasichana wakimbizi nchini Kenya; Harakati za kuhamishia wakimbizi wa DRC nchini Burundi kuelekea maeneo salama; mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni kwa wanawake na wasichana.Kwenye mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu  Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani, akionya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Ripoti yake Anold Kayanda.Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.Ripoti yake Sharon Jebiichi.Makala Assumpta Massoi anakupeleka mpakani mwa Burundi na Jamhuri ya Ki

  • Kutana na Celestin Mbaruku mkimbizi mnufaika wa Mpango wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali nchini Kenya

    28/02/2025 Duración: 03min

    Kama mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Celestin Mbaruku hakuwa na fursa ya ajira rasmi hadi alipothibitishwa ujuzi wake kupitia mpango wa Serikali ya Kenya wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali, uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO.Kupitia ILO Celestin Mbaruku ni mnufaika wa ufadhili wa PROSPECTS, ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao.Kimakosa, Celestin Mbaruku akiwa nchini mwake DRC alidhaniwa kuwa muasi, akafungwa lakini akamudu kutoroka hadi Kenya.Kabla ya masaibu haya, huko DRC alikuwa Mwalimu anayesimamia nidhamu katika shule alikokuwa anafanya kazi ya lakini kwa kuwa vyeti vyake vilipotea, hata alipovuka kuingia Kenya, hakuwa na uthibitisho wa kiwango cha elimu yake licha ya kuwa ana diploma ya mbinu za ufundishaji.Na hapo ndipo ikabidi achomoe kibin

  • Guterres: Mwezi Mtukufu wa Ramadhani utumike kuleta amani

    28/02/2025 Duración: 02min

    Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwishoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe wake wa kutaka kipindi hicho cha takribani siku 30 kitumike kuleta amani na kuongoza kuelekea dunia yenye yenye haki na huruma zaidi. Selina Jerobon na taarifa zaidi.

  • 28 FEBRUARI 2025

    28/02/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia migogoro ambayo yameendelee kwa muda mrefu Sudan Kusini, na ujumbe wa Katibu Mkuu ikielekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Makala inatupeleka nchini Kenya, na mashinani nchini Tanzania.Viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo.Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwishoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe wake wa kutaka kipindi hicho cha takribani siku 30 kitumike kuleta amani na kuongoza kuelekea dunia yenye yenye haki na huruma zaidi..Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii kutokana na video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, anakupeleka nchini Kenya kukutanisha na mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC am

  • Viongozi wabainika kuwa chanzo cha kutomalizika kwa mzozo nchini Sudan Kusini

    28/02/2025 Duración: 02min

    Viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo kama anavyoripoti Flora Nducha.

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Fahari isiyo pari haina heri"

    27/02/2025 Duración: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “FAHARI ISIYO PARI HAINA HERI.”.

  • 27 FEBRUARI 2025

    27/02/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini DRC ambako leo tunamulika mmoja wa raia aliyerejea makazi yake huko Sake, nje kidogo ya mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini baada ya waasi wa M23 kutangaza kuwa wakimbizi wote wa ndani lazima warejee vijijini kwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Ikiwa ni mwezi mmoja sasa tangu waasi wa M23 watwae mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kuendelea kutwaa miji mingine huku mamia ya maelfu ya watu wakifurushwa makwao, hii leo mashirika ya Kibinadamu nchini humo yametoa ombi la dola bilioni 2.54 ili kusaidia watu milioni 11 walioathiriwa vibaya na mzozo unaoendelea.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO Dkt. Tedros Ghebreysus ametangaza kuwa ugonjwa wa mpox bado ni tishio la afya ya umma duniani na hivyo nchi lazima ziendelee kuwa makini katika ufuatiliaji, uchunguzi, kinga na matibabu.Na kuelekea Mkutano wa viongozi kuhusu Mifumo ya uzalishaji

  • Hatari ya watu milioni 4.4 nchini Somalia kukumbwa na njaa mwezi Aprili mwaka huu

    26/02/2025 Duración: 02min

    Watu milioni 4.4 nchini Somalia wako hatarini kukumbwa na njaa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, kutokana na ukame mkali, mizozo na ongezeko kubwa la bei za vyakula. Selina Jerobon na taarifa zaidi..

  • 26 FEBRUARI 2025

    26/02/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu nchini Somalia na huduma zaa faya kwa wakimbizi wajawazito nchini Chad. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Uganda, kulikoni?Watu milioni 4.4 nchini Somalia wako hatarini kukumbwa na njaa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, kutokana na ukame mkali, mizozo na ongezeko kubwa la bei za vyakula.Nchini Chad, taifa lililoko kaskazini-kati mwa Afrika mkunga mmoja amehamia kwa muda katika kambi ya wakimbizi ili kuhakikisha wajawazito wanapata huduma bora kabla na baada ya kujifungua kama njia mojawapo ya kuepusha vifo vya wajawazito na watoto wachanga.Makala inatupeleka nchini Kenya kumulika mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, wa kulinda lishe ya wasiojiweza unavyoleta mabadiliko katika  jamii kuanzia kaunti ya Turkana hadi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma.Katika mashinani fursa ni yake Dkt Annett Alenyo Ngabirano kutoka Uganda akisema juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO na Wizara ya Afya ya Ug

  • Mradi wa FAO wa kulinda lishe ya wasiojiweza umekuwa mkombozi Turkana nchini Kenya

    26/02/2025 Duración: 04min

    Mradi unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, wa kulinda lishe ya wasiojiweza wakiwemo wajasiriamali wa bishara ndogodogo na za kati, wakulima wadogo wa matunda na mbogamboga, wafugaji  na wachuuzi wa samaki kama sehemu ya jitihada za kujikwamua baada ya janga la COVID-19 umeleta nuru kwa jamii mbalimbali ikiwemo katika kaunti ya Turkana Kaskazini Magharibi mwa Kenya na katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma. Je unawanufaisha vipi wakulima na kwa nini ni muhimu? Ungana na Flora Nducha katika makala hii kwa undani zaidi

  • Mkunga apiga kambi kwa wakimbizi ili kuepusha vifo vya wajawazito - Chad

    26/02/2025 Duración: 01min

    Nchini Chad, taifa lililoko kaskazini-kati mwa Afrika mkunga mmoja amehamia kwa muda katika kambi ya wakimbizi ili kuhakikisha wajawazito wanapata huduma bora kabla na baada ya kujifungua kama njia mojawapo ya kuepusha vifo vya wajawazito na watoto wachanga. Taarifa ya Evarist Mapesa inafafanua zaidi.

página 4 de 5