Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 9:04:30
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • UNRWA: Hakuna popote na yeyote aliye salama Gaza ni zahma kila mahali

    15/09/2025 Duración: 02min

    Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Philippe Lazzarini, ametoa onyo kali kuwa “hakuna sehemu yoyote iliyo salama Gaza, na hakuna mtu aliye salama”akisema  zahma na madhila  yametanda kila kona ya eneo hilo linalokaliwa kimabavu na Israel. Flora Nducha na taarifa zaidi

  • Asante UNMISS sasa kesi za miaka 10 zinaenda kusikilizwa

    15/09/2025 Duración: 03min

    Nchini Sudan Kusini ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendelea kuimarisha mfumo wa mahakama ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wote hata maeneo yote ya nchi hiyo. Leah Mushi na taarifa zaidi

  • 15 SEPTEMBA 2025

    15/09/2025 Duración: 10min

    Jaridani leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, haki za binadamu nchini Sudan Kusini na ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya demokrasia duniani.Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Philippe Lazzarini, ametoa onyo kali kuwa “hakuna sehemu yoyote iliyo salama Gaza, na hakuna mtu aliye salama”akisema      zahma na madhila  yametanda kila kona ya eneo hilo linalokaliwa kimabavu na Israel.Leo ni siku ya demokrasia duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameeleza bayana kuwa demokrasia iko hatarini duniani.Nchini Sudan Kusini ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendelea kuimarisha mfumo wa mahakama ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wote hata maeneo yote ya nchi hiyo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

  • Demokrasia inayotenga katu si demokrasia - Guterres

    15/09/2025 Duración: 02min

    Leo ni siku ya demokrasia duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameeleza bayana kuwa demokrasia iko hatarini duniani. Asumpta Massoi na taarifa zaidi.

  • Kengele ya amani yagongwa UN kuikumbusha dunia wakati wa kuchua hatua kuidumisha ni sasa: Guterres

    12/09/2025 Duración: 03min

    Leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani hafla maalum imefanyika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani ambayo kwa kawaida huwa kila mwaka tarehe 21 Septemba. Katibu Mkuu António Guterres katika hafla hiyo ameisihi dunia ambayo imeghubikwa na vita na machafuko kila kona kuwa wakati ni sasa kuchukua hatua na kutimiza ndoto ya amani iliyoanza mwaka 1945 baada ya vita vya pili vya dunia. Flora Nducha amefuatilia hafla hiyo na kutuandalia taarifa hii. Karibu Flora(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Natts --bellLeo, mlio mzito wa Kengele ya Amani umesikika kwenye Makao Makuu ya Umoja wakati wa hafla hiyo iliyoambatana na na burudani ya muziki wa allaNatts........Kisha Katibu Mkuu Guterres akawageukia washiriki na kusema “miaka ni themanini iliyopita Umoja wa Mataifa kuzaliwakutoka kwenye majivu ya vita ili kusaka amani”, akatoa ujumbe ulio wazi,sasa  jukumu la amani duniani ni la dharura kuliko wakati mwingine wowote.Wakati migogoro ikienea na mamilioni ya raia wakiendelea kunaswa kwenye

  • Mshikamano wa nchi zinazoendelea kuchagiza SDGs

    12/09/2025 Duración: 02min

    Leo ni siku ya kimataifa ya ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea zikijulikana pia kama nchi za kusini ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa tamko lenye msukumo mkubwa likitambua ustahimilivu, ubunifu, na ushawishi unaoongezeka wa nchi zinazoendelea katika kuleta maendeleo ya kimataifa. Assumpta Massoi anatoa maelezo zaidi.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Kwanza kabisa ni vema kufahamu kuwa nchi hizi zinaitwa za kusini, kwa maana kwamba bado ziko nyuma kimaendeleo zikilinganishwa na zile za kaskazini, (ingawa si kijiografia) ambazo zinaonekana kuwa zina maendeleo kiuchumi.Maudhui ya siku hii ni – fursa mpya na ubunifu kupitia ushirikiano wa kusini-kusini na ushirikiano wa pembetatu, ikimaanisha ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea, na vile vile mashirika ya kimataifa na nchi zilizoendelea.Sasa katika siku hii ya leo iliyopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 22 mwezi Desemba mwaka 2003 kwa lengo la kusongesha ushirikiano wa kiufundi baina ya nchi zinazoendelea Guterres an

  • UNICEF yawawezesha vijana kwenye kilimo nchini Kenya

    12/09/2025 Duración: 03min

    Kaunti ya Kirinyaga, iliyoko katikati mwa nchi ya Kenya kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, inashuhudia mageuzi mapya katika sekta ya kilimo kupitia mradi wa kuwahusisha vijana  katika kilimo na lishe unaojulikana kama EKYAN. Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na wadau nchini humo.  Karibu Sabrina Saidi utupe taarifa zaidi.....(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Mradi wa EKYAN ni mfano wa ujasiriamali wa kilimo unaoongozwa na vijana, ukiwa na lengo la kutengeneza fursa za ajira, kuwanufaisha na kubadilisha maisha ya vijana walioko vijijini, kupitia mbinu bora za kilimo na lishe, ukitekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, serikali ya kaunti ya Kirinyaga na shirika linalotoa mafunzo, elimu ya biashara ndogo ndogo na uwezeshaji barani Afrika KUZA Biashara.Felista Nyakio Mutungi kijana mkulima wa kaunti ya Kirinyaga, ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo kupitia mradi huo. Na h

  • 12 Septemba 2025

    12/09/2025 Duración: 11min

    Karibu usikilize jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo tunaangazia masuala ya amani pamoja na ushirikiano wa nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea duniani. Pia utasikia habari kutoka mashinani nchini Kenya kuhusu mradi wa UNICEF kwenye kilimo uliowainua kiuchumi vijana. Mtangazaji wako ni Leah Mushi. 

  • 11 SEPTEMBA 2025

    11/09/2025 Duración: 09min

    Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuletea-Utapiamlo kwa watoto katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel umefikia kiwango cha kutisha, huku takwimu mpya zikionesha ongezeko kubwa mwezi Agosti kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa-Umoja wa Mataifa umeanzisha mradi mpya wa miaka mitatu wenye lengo la kusaidia nchi za Afrika Mashariki kukabiliana na matumizi ya kigaidi ya vilipuzi. Kupitia mradi huu, Kenya, Somalia na Uganda zitasaidiwa-Hali nchini Haiti inaendelea kuzorota, sehemu kubwa ya nchi inadhibitiwa na magenge yenye silaha, nusu ya idadi ya watu wanakabiliwa na upungufu wa chakula, na idadi ya watu waliofurushwa  imefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa amesema Tom Fletshe mkuu wa OCHA-Mada kwa kina inatupeleka Uganda watumiaji wa Ziwa Albert wafunguka kuhusu changamoto za uvuvi haramu na faida za ziwa hilo-Na katika jifunze KIswahili leo mtaalam wetu Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzi

  • Harakati za UN na serikali ya Uganda kukabili tabianchi huko Karamoja

    10/09/2025 Duración: 02min

    Karamoja, eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda, linakabiliwa na changamoto kubwa za tabianchi kama vile ukame wa mara kwa mara na milipuko ya magonjwa ya mimea na mifugo, hali inayotishia uhakika wa chakula. Kupitia mradi wa PROACT, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la  Chakula na Kilimo Duniani (FAO), na Mpango wa chakula Duniani (WFP) pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya, EU, wameshirikiana katika kuimarisha mifumo ya kushughulikia mabadiliko ya kiikolojia na kijamii. Anold Kayanda na maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda) Video iliyoandaliwa na FAO inaanza ikionesha wana jamii katika eneo la Karamoja wanavyojihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kilimo na ufugaji licha ya changamoto za tabianchi.  Dustan Balaba Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Uganda anaeleza kuhusu mradi huu mpya akisema,"Wadau wameweza kuhakikisha kwamba kuna maendeleo ya haraka katika upatikanaji wa taarifa na tunatumia maendeleo ya kiteknolojia kwa m

  • Kwa mara ya kwanza watoto wenye utipwatipwa duniani ni wengi kuliko wenye utapiamlo

    10/09/2025 Duración: 02min

    Kwa mara ya kwanza idadi ya watoto na vijana wa umri wa kwenda shule wenye unene wa kupindukiaau utipwatipwa imezidi idadi ya watoto wenye utapiamlo duniani ikiathiri watoto milioni 188 sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto 10 imesema leo ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tuungane na Leah Mushi kusikia zaidi kuhusu ripoti hiyo, karibu LeahRipoti hii mpya ya UNICEF iitwayo “Faida kwenye vyakula: Jinsi Mazingira ya Chakula yanavyowaangusha watoto” imechambua takwimu kutoka nchi zaidi ya 190 na kubaini kwamba kiwango cha watoto wenye utapiamlo kimepungua tangu mwaka 2000, lakini wale wenye unene wa kupindukia kimeongezeka mara tatu.Kwa sasa, utipwatipwa umeenea katika kila eneo la dunia isipokuwa Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia Kusini. Nchi za visiwa vidogo vya Pasifiki ndizo zinaongoza kwa kuwa na viwango vya juu zaidi, ikiwemo Niue yenye asilimia 38 ya watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 19 wakiwa na unene wa kupindukia.Nin

  • Türk ataka uwajibikaji wa vikosi vya usalama Nepal na waandamanaji wazingatie kanuni

    10/09/2025 Duración: 02min

    Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu ameonesha wasiwasi mkubwa kufuatia ghasia zinazoendelea na kushika kasi nchini Nepal, huko barani Asia, ambako maandamano dhidi ya ufisadi na marufuku ya mitandao ya kijamii yamesababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi. Flora Nducha amefuatilia taarifa hiyo na anatupasha zaidi.Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, akizungumza mjini Geneva amesema“nimeshtushwa na ongezeko la ghasia nchini Nepal ambalo limesababisha vifo kadhaa na kujeruhi mamia ya waandamanaji wengi wao wakiwa vijana, pamoja na uharibifu mkubwa wa mali.”Katika siku za karibuni, maandamano yaliyoanzia katika mji mkuu Kathmandu sasa yamesambaa katika miji na vijiji vya Nepal, yakiacha barabara zikifunikwa na mabaki ya vitu vilivyoteketezwa kwa moto na kulazimisha maduka kufungwa pia kuhofia usalama.Kwa mujibu wa duru za habari maandamano hayo yanayoo nngozwa na vijana wa kati ya umri wa miaka 13 hadi 28 au Gen Z yameshakatili Maisha ya takribani watu

  • 10 SEPTEMBA 2025

    10/09/2025 Duración: 10min

    Leo jaridani Assumpta Massoi anamulika kauli ya OHCHR kufuatia maandamano yanayoendelea Nepal; Utipwatipwa 'wapiku' utapiamlo na harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huko Karamoja nchini Uganda,Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu ameonesha wasiwasi mkubwa kufuatia ghasia zinazoendelea na kushika kasi nchini Nepal, huko barani Asia, ambako maandamano dhidi ya ufisadi na marufuku ya mitandao ya kijamii yamesababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi. Flora Nducha amefuatilia taarifa hiyo na anatupasha zaidi.Kwa mara ya kwanza idadi ya watoto na vijana wa umri wa kwenda shule wenye unene wa kupindukiaau utipwatipwa imezidi idadi ya watoto wenye utapiamlo duniani ikiathiri watoto milioni 188 sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto 10 imesema leo ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tuungane na Leah Mushi kusikia zaidi kuhusu ripoti hiyo, karibu LeahKaramoja, eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda, linakabiliwa na chan

  • 09 SEPTEMBA 2025

    09/09/2025 Duración: 09min

    -Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea UNGA79yafikia tamati hii leo na kupisha UNGA80  chini ya uongozi wa Rais mpya Annalena Baerbock-Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyozinduliwa leo imesema matumizi ya kijeshi duniani yalifikia dola trilioni 2.7 mwaka 2024, yakiwa yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 9 kutoka mwaka 2023-Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher ametangaza leo  dola milioni 1 za kimarekani kutoka  Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa CERF ili kudhibiti mlipuko wa kipindupindu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. -Mada kwa kina inatupeka Pemba Kaskazini kisiwani Zanzibar nchini Tanzania kuangazia mradi wa FAo wa ZJP unavobadili maisha ya wakulima wa ndiziNa katika jifunze Kiswahili utamsikia mlumbi Jorum Nkumbi kutoka Tanzania akifafanua maana ya neno LISANI

  • Shirika la Umoja wa Mataifa la afya,WHO laongeza orodha ya dawa muhimu

    08/09/2025 Duración: 03min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limefanya mabadiliko muhimu katika orodha yake ya dawa muhimu duniani au Essential Medicines List – EML na orodha ya dawa muhimu kwa watoto (EMLc) ikijumuisha dawa za kisasa za saratani, kisukari, unene uliopitiliza na magonjwa mengine sugu.Orodha za WHO za dawa muhimu ni nyenzo za mwongozo zinazotumiwa na zaidi ya nchi 150 kupanga ununuzi, bima za afya na upatikanaji wa dawa. Kwa lugha rahisi, dawa zinazoorodheshwa hapa huwa na nafasi kubwa zaidi ya kununuliwa na kutolewa kwa wagonjwa kupitia huduma za umma kwani wanachama wa WHO wanaziweka dawa hizi kama kipaumbele cha kiafya kwa mamilioni ya watu duniani.WHO wakati wakitangaza orodha hiyo mpya waliweka bayana kuwa dawa hizi mpya si za majaribio, bali ni zile ambazo zimethibitishwa kitabibu kuwa zinaokoa maisha, kupunguza madhara ya magonjwa na kuboresha maisha ya wagonjwa.Nini maana yake?Kuongezwa kwa dawa hizi ni hatua ya mbele katika safari ya kuhakikisha afya bora kwa wote. Inamaanisha wagonjwa zaidi wa sa

  • Wanavyosema wadau kuhusu Siku ya kujua kusoma na kuandika katika zama za kidijitali

    08/09/2025 Duración: 02min

    Ikiwa leo tarehe 8 Septemba ni siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ambapo Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hii ili kuwakumbusha watunga sera, walimu, wadau wa elimu, na jamii juu ya umuhimu wa ujuzi wa kusoma na kuandika katika kujenga jamii yenye elimu, haki, amani na endelevu,  Sabrina Saidi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anaiangazia kauli mbiu ya mwaka huu  "Kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika katika zama za kidijitali" akiwashirikisha baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania.Amezungumza na baadhi ya wadau kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT kilichoko jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania.Dismas Nziku ni mwalimu wa masomo ya Biashara na Ujasiriamali  anazungumza kuhusu ni kwa jinsi gani ufundishaji wa zama hizi za kidijitali unavyochochea na kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika. "Kwenye dunia ya sasa ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali ni msingi mkubwa kwa mwanafunzi, na miongoni mwa juzi hizi muhimu ni kama vile kujua kutumia vifaa vya kidijit

  • Lacroix: Heko MONUSCO na FARDC kwa kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha

    08/09/2025 Duración: 02min

    Huko Bunia, jimboni Ituri Mashariki Mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC,  Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, amepongeza juhudi za pamoja za walinda amani wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO na jeshi la serikali ya Congo, FARDC, katika juhudi za kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha.Akizungumza wakati wa ziara yake iliyoanza Septemba 6, Mashariki mwa DRC katika jimbo la Ituri Lacroix amesema ushirikiano na kuaminiana kati ya mamlaka za jimbo la Ituri na vikosi vya Umoja wa Mataifa ni msingi muhimu wa kurejesha amani.Anasema “Nipo katika eneo liitwalo Fataki, katika jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na hapa kuna kambi ya MONUSCO yenye kikosi cha Nepal, pamoja na kambi ya wakimbizi wa ndani. Maelfu ya watu wanalindwa hapa na wenzetu wa MONUSCO, na wanapatiwa msaada wa kibinadamu pamoja na ulinzi.”Gavana wa Ituri, Jenerali Johnny Luboya, alikaribisha msaada wa MONUSCO katika operesheni za kijes

  • 08 SEPTEMBA 2025

    08/09/2025 Duración: 09min

    Heko MONUSCO na FARDC kwa kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha: LacroixSiku ya kimataifa ya kujua kusoma na kuandika.WHO yatoa orodha ya dawa muhimu duniani.

  • MINUSCA washiriki kutoa elimu ya usalama barabarani CAR

    05/09/2025 Duración: 02min

    Kila mwaka,Wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji wa Anga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR,  kwa msaada wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MINUSCA,huandaa kampeni za usalama barabarani. Na hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo,Bangui, MINUSCA kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya Ndani ISF wameungana kupambana na ajali za barabarani zinazoongezeka kila uchao,doria ya pamoja imefanyika kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara. Sabrina Saidi anatujuza zaidi....​(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Natts ....ongeza hii; katikaa mitaa ya Banguimji mji mkuu wa CAR pisha nikupishe ni nyingi. Kufuatia ongezeko la ajali za barabarani,zinazopoteza maisha ya watu kila uchao, kikosi cha polisi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA kimeendesha doria ya pamoja ya usalama kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya nchi hii (ISF) katika mji mkuu BanguiOperesheni hii iliyofanyika tarehe 4 mwezi Septemba,mwaka huu imelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki za abiria maarufu

  • UNICEF: Mateso kwa watoto wa Gaza ni bayana

    05/09/2025 Duración: 02min

    Sasa twende Gaza, hii ni hadithi ya maisha, ya watoto wa Gaza wanaokabiliana na baa la njaa, hofu, na kuporomoka kwa kila kitu kinachowaweka hai. Ni hadithi inayoelezwa kupitia macho ya wale wanaoshuhudia mateso kila siku wakiwemo madaktari, akina mama, na wahudumu wa kibinadamu wanaopiga kengele ya tahadhari. Miongoni mwa wahudumu hao ni Tess Ingram afisa mawasiliano wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ofisi ya Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Flora Nducha anasimulia alichokishudia(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Tess aliyefunga safari na kushuhudia hali halisi Gaza akizungumza na waandishi wa habari kutoka mji wa Al Mawasi amesema mwenye macho haambiwi tazama na alichokishuhudia ni cha kutisha kwani jiji hilo sasa linazidi kuzama kwenye lindi la baa la njaa, vituo vya lishe vimefungwa, familia zinalia na kuhaha na watoto wanakufa kila uchao bila msaada.(Tess Ingram- Sheillah)“Jiji la Gaza, kimbilio la mwisho kwa familia za Kaskazini, linakuwa mahali ambapo utoto hauwezi kuishi.&

página 3 de 5