Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:55:34
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Jifunze Kiswahili: maana ya neno KIHEREHERE

    05/06/2025 Duración: 45s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno KIHEREHERE.

  • 05 JUNI 2025

    05/06/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo ikiwa ni siku ya mazingira duniani mwaka ikibeba maudhui “Tokomeza taka za Plastiki,” tunakwenda Tanzania kumsikia Clara Makenya, Mkua wa UNEP nchini humo na afisa mawasiliano wa shirika hilo kwa ajili ya Namibia akizungumza kuhusu changamoto ya taka za plastiki Tanzania na nini kifanyike kuzitokomeza.Naanzia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani ambapo leo kumefanyika tukio maalum la kukumbuka na kuenzi watumishi 168 wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi wa amani, haki, na usaidizi, Mishumaa iliwashwa na kisha walitajwa majina yao mmoja baada ya mwingine akiwemo Nats.. mlinda amani wa UN kutoka Tanzania. Wanafamilia walipokea tuzo maalum za kutambua mchango wao.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mazingira, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka hatua za dharura kutokomeza janga la uchafuzi utokanao na taka za plastiki, akilitaja kama “janga” linaloikaba dunia na kutishia afya ya binad

  • Uwekezaji sahihi ni ule unaoanzia kwa wananchi na si ngazi ya juu - Madina

    04/06/2025 Duración: 02min

    Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki. 

  • 04 JUNI 2025

    04/06/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia haki za jamii za Ogiek nchini Kenya, na masuala ya baharí na tabianchi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Mtaalamu wa UN ataka kusitishwa mara moja kwa uwekaji  mipaka unaotishia haki za Waogiek Kenya. Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaka Serikali ya Kenya kusitisha mara moja shughuli za uwekaji mipaka katika Msitu wa Mau Mashariki nchini humo, akisema kuwa unakiuka haki za jamii ya asili ya Waogiek na kupuuza maamuzi ya lazima ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR).Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki. Akiwa huko Hamburg nimemuuliza Madina ni kipi amejulisha washiriki wenzake kuwa kinapaswa kufanyika ili dunia iwe endelevu?.Makala, katika

  • Kuelekea Mkutano wa Bahari UNOC3, UNEP yatoa wito wa hatua za kukabili taka za plastiki

    04/06/2025 Duración: 03min

    Katika kuelekea Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari UNOC3, utakaofanyika mjini Nice, Ufaransa kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025, Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa bahari, hasa wa taka za plastiki. Akizungumza na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNIC jijini Dar es Salaam, Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, alisisitiza umuhimu wa kushughulikia kwa haraka tatizo la taka za plastiki ambazo nyingi hutokea nchi kavu na kuishia baharini.

  • Mtaalamu wa UN ataka kusitishwa mara moja kwa uwekaji mipaka unaotishia haki za Waogiek nchini Kenya

    04/06/2025 Duración: 01min

    Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaka Serikali ya Kenya kusitisha mara moja shughuli za uwekaji mipaka katika Msitu wa Mau Mashariki nchini humo, akisema kuwa unakiuka haki za jamii ya asili ya Waogiek na kupuuza uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR). Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • 03 JUNI 2025

    03/06/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kinainayomulika kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi katika kaunti kama Kajiado, Kenya, ambayo jamii hukumbwa na hali ya ukame na mazingira magumu, mabadiliko chanya yanaonekana.Mustakabali wa mzingiro wa Israeli kwenye eneo la Palestina la Gaza inalokalia kimabavu ukiendelea kukumbwa na sintofahamu, wanawake na wasichana wamesimulia adha ya ukosefu taulo za kike wakati wanapokuwa kwenye hedhi huku upatikanaji wa maji ukiwa ni wa taabu.Idadi ya wakazi wa nchi zenye maendeleo duni, LDCs na zile za visiwa vidogo, SIDS  wanaopata huduma zilizoboreshwa au za kisasa za maonyo ya mapema kabla ya majanga imefikia takribani milioni 400 na hii ni kutokana na programu ya CREWS iliyoanzishwa mwaka 2015 na shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO.Rebecca Kalonji, al maaruf Sista Becky, mwimbaji chipukizi wa mtindo wa kufokafoka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hii leo ametangazwa kuwa Muungano Mkono wa Ngazi ya Juu wa masuala ya lishe na ulaji wenye a

  • Shirika la kiraia lawezesha vijana wa kike kujiajiri badala ya kutumbukia kwenye umaskini

    02/06/2025 Duración: 03min

    Nchini Tanzania ugumu wa maisha na kukabiliwa na vishawishi, umewapa fikra mpya vijana wa kike mkoani Morogoro, mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambao sasa wanajimudu kiuchumi,  kwa kuanzisha biashara na shughuli za ujasiriamali. Wanasongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan namba 8 la ajira zenye staha, nan amba 1 la kutokomeza umaskini. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time FM amewatembelea vijana hao na kuandaa makala hii.

  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashutumu mashambulizi dhidi ya Wapalestina wanaotafuta msaada

    02/06/2025 Duración: 01min

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza kughadhabishwa kufuatia kusambuliwa, kujeruhiwa na kuuawa kwa Wapalestina walipokuwa wakijaribu kupata msaada wa kibinadamu huko Gaza jana Jumapili, Juni Mosi. Selina Jerobon na taarifa zaidi.

  • 02 JUNI 2025

    02/06/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia haki za kibidamu katika ukanda wa Gaza, na hali ya misaada ya kibinadamu huko huko Gaza. Makala yunakwenda nchini Tanzania kusikia harakati za kusaidia vijana wa kike, na mashinani tunakupeleka nchini Uganda kusikia kuhusu mradi wa mlo shuleni.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza kughadhabishwa kufuatia kusambuliwa, kujeruhiwa na kuuawa kwa Wapalestina walipokuwa wakijaribu kupata msaada wa kibinadamu huko Gaza jana Jumapili, Juni Mosi.Maisha ya raia wa Gaza ambao karibu wote ni wakimbizi wa ndani yanazidi kuwa mtihani usio na majawabu kila uchao kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Mateso wanayopitia nis awa na kuishi jrehanamu, wengi wamekata tamaa na wanaona bora kufa kuliko kuishi katika hali hiyo. Flora Nducha akusimulia madhila ya mmoja wa wakimbizi hao wa ndani Moamen Abu Asr na mkewe Zeinat..  Makala inakupeleka nchini Tanzania kusikia harakati za kunasua vijana wa kike kutoka vishawishi vinavyoweza kuwatumbukiza kwenye lindi

  • Tumefika mwisho, ni bora kufa kuliko mateso haya: Wakimbizi Gaza

    02/06/2025 Duración: 02min

    Maisha ya raia wa Gaza ambao karibu wote ni wakimbizi wa ndani yanazidi kuwa mtihani usio na majawabu kila uchao kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Mateso wanayopitia nis awa na kuishi jrehanamu, wengi wamekata tamaa na wanaona bora kufa kuliko kuishi katika hali hiyo. Flora Nducha akusimulia madhila ya mmoja wa wakimbizi hao wa ndani Moamen Abu Asr na mkewe Zeinat. 

  • Walinda amani kutoka Tanzania TANZBATT 11 wajivunia kazi zao za kuwaunga mkono raia DRC

    30/05/2025 Duración: 02min

    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC jimboni Kivu Kaskazini katika kitongoji cha Mavivi tunakutana na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 11, TANZBATT11, wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wakielezea sio tu majukumu yao, bali pia wanajivunia kile wanachofanya kwa kuzingatia Mei 29 imeadhimishwa siku ya kimataifa ya walinda amani. Afisa Habari wa TANZBATT 11 Meja Fadhila Nayopa amefuatilia hadithi zao. 

  • Licha ya ukata UNICEF yajitahidi watoto nchini DRC warejee shuleni

    30/05/2025 Duración: 02min

    Wakati ghasia zinazoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinaripotiwa kusababisha zaidi ya watoto milioni 1.8 kutokuweko shuleni, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini humo linajitahidi kwa udi na uvumba kuhakikisha watoto wanapata elimu kwani ni haki yao ya msingi. Je ni kwa vipi? Anold Kayanda anasimulia zaidi.

  • 30 MEI 2025

    30/05/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya elimu kwa watoto mashariki mwa DRC na Mkutano wa pili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT unaofunga pazia leo jijini Nairobi Kenya. Makala inaturejesha nchini DRC na mashinani inatupeleka katika bonde la Ziwa Victoria, kulikoni?Wakati ghasia zinazoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinaripotiwa kusababisha zaidi ya watoto milioni 1.8 kutokuweko shuleni, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini humo linajitahidi kwa udi na uvumba kuhakikisha watoto wanapata elimu kwani ni haki yao ya msingi.Mkutano wa pili wa siku mbili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT leo unafunga pazia jijini Nairobi Kenya. Baraza hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne ni chombo cha juu kabisa duniani cha kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya miji endelevu na limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau m

  • Malawi inachukua hatua madhubuti kukabiliana na changamoto za makazi - Mercy Bety Dube

    30/05/2025 Duración: 02min

    Mkutano wa pili wa siku mbili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT leo unafunga pazia jijini Nairobi Kenya. Baraza hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne ni chombo cha juu kabisa duniani cha kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya miji endelevu na limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau mbalimbali wa amendeleo ya miji. Flora Nducha na taarifa zaidi.

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MISHEMISHE.”

    29/05/2025 Duración: 38s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi  Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "MISHEMISHE.”

  • 29 MEI 2025

    29/05/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa ikitupeleka nchini DRC, Sierra Leone na Ghana. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na maana ya neno "MISHEMISHE.”Leo ni Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani ambayo mwaka huu inajikita na maudhui ya “mustakabali wa ulinzi wa amani.”Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema walinda amani wa Umoja wa Matafa wako katika changamoto kubwa “Leo hii, walinda amani wanakabiliwa na hali zinazozidi kuwa ngumu katika dunia inayozidi kuwa na changamoto, ikiwemo uugawanyika na kutofautiana kwa mitazamo duniani kunazidi kuongezeka, operesheni za ulinzi wa amani zinakabiliwa, hatari zaidi kutokana na wingi wa vitisho kama vile ugaidi na walinda amani kulengwa kwa makusudi kupitia taarifa potofu zenye madhara makubwa na changamoto zinazovuka mipaka kuanzia janga la mabadiliko ya tabianchi hadi uhalifu wa kimataifa.Kikosi cha 11 cha Tanzania kinachohudumu chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchi

  • Walinda amani wa UN kutoka Mongolia waokoa wakazi wa Abiemnhom nchini Sudan Kusini

    28/05/2025 Duración: 02min

    Kuelekea siku ya walinda amani Mei 29, tunakwenda nchini Sudan Kusini kumulika walinda amani na ulinzi wa raia. Katika taifa hilo changa zaidi duniani  walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Mongolia wanaohudumu kwenye Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (UNMISS) walikuwa msaada mkubwa wakati kijiji cha Abiemnhom kaskazini mwa Sudan Kusini kilipovamiwa. Walinda amani hao walifika haraka  kutoka kituo chao cha karibu na kutoa msaada wa kuokoa manusura na miili ya waliouawa. Je nini kilifanyika zaidi Sharon Jebichii anasimulia kwenye makala hii iliyotokana na video ya UNMISS.

  • Ukraine: Mashambulizi ya Urusi dhidi ya raia kwa kutumia ndege zisizo na rubani yaangaziwa

    28/05/2025 Duración: 01min

    Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imehitimisha kwamba vikosi vya kijeshi vya Urusi vimetenda uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, hasa mauaji, kupitia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drones) yaliyoelekezwa dhidi ya raia. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • 28 MEI 2025

    28/05/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu nchini Ukraine na upatikanaji wa elimu nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Sudan Kusini, na amashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imehitimisha kwamba vikosi vya kijeshi vya Urusi vimetenda uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, hasa mauaji, kupitia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drones) yaliyoelekezwa dhidi ya raia.Mradi wa "operesheni rejea shuleni" unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na wizara ya elimu ya Kenya, shirika liliso la kiserikali la Hapag Lloyd na wadau wengine kwa kuzipa fedha familia zisizojiweza kuendesha shughuli za kiuchumi, umerejesha mautumaini ya elimu kwa mamia ya watoto katika Kaunti ya Kwale Pwani ya Kenya  ambao waliacha shule sababu ya umasikini.  Katika makala ikielekea siku ya walinda amani kesho Mei 29, tunamulika harakati za walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini S

página 1 de 5