Habari Za Un

01 OKTOBA 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Wazee duniani na mchango wao kwa jamii, hali ya afya katika ukanda wa Gaza, na simulizi ya Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako kumefanyika tukio maalum la kuadhimisha siku ya wazee duniani leo Oktoba Mosi, kaulimbiu ikiwa Wazee Wanaendesha Hatua za Kijamii na Kimaisha: Matamanio Yetu, Ustawi Wetu na Haki Zetu. Anayekupeleka ukumbini ni Flora Nducha.Huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanawake katika eneo la Deir al- Balah wanalazimika kutumia majiko ambayo wanachochea taka za plastiki na makaratasi ili kupota moto wa kuweza kupikia chakula. Hali hiyo imesababisha kuenea kwa magonjwa ya kupumua kama vile numonia na pumu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linatoa wito kwa viongozi wa Afrika kufanya uwekezaji wa kifedha wa busara utakaowezesha watoto kupata ujuzi wa msingi wa kujifunza na mustakabali wenye nguvu kwa bara la Afrika. Balozi Mwema wa UNICEF, Angeli