Habari Za Un

Ili Afrika ‘iimarike kiafya’ inabidi isiwe tegemezi kwenye masuala ya kifedha: Dkt. Ntuli Kapologwe

Informações:

Sinopsis

Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masuala mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano  wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya. Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza tena na Dkt. Kapologwe mara tu baada ya mkutano huo