Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
Maandamano ya vijana wa Gen Z nchini Kenya kulalamikia kupanda kwa bei ya mafuta
21/04/2026 Duración: 09min -
makubaliano mapaya kati ya Serikali ya DRC na M23 kukubaliana
20/04/2026 Duración: 10minSerikali ya DRC na waasi wa M23, mwishoni mwa juma wamekubaliana kuruhusu misaada ya kibinadamu kufika kwenye maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo pamoja na kubadilishana wafungwa katika muda wa siku 10 zijazo, haya yakifuatia mazungumzo ya Uswis yalitoratibiwa
-
-
-
Uhaba na bei za juu za mafuta zashuhudia kashfa ya maofisa wa serikali kuhodhi
08/04/2026 Duración: 10min -
DRC kuanza kuwapokea wakimbizi haramu kutoka Marekani katika mkataba maalum
07/04/2026 Duración: 10min -
Africa : Mila za Africa je zinapotea ?
04/04/2026 Duración: 09minKatika makala haya tunajadili iwapo mila za kiafrica zimeanza kuweka na namna gani zinaweza kudumishwa. Skiza makalaa
-
Maoni ya waskilizaji kuhusu matangazo yatu juma hili
03/04/2026 Duración: 09minKila Ijumaa rfi Kiswahili inakuapa fursa kuchangia mada yoyote ile. Skiza maoni ya juma hili.
-
DRC : Yafunzu kucheza Kombe la Dunia 2026
01/04/2026 Duración: 09minDRC imejikatia tiketi ya kucheza kwenye kupute cha kuwania kombe la dunia Haya hapa maoni ya waskilizaji.
-
Kombe la Dunia : Hofu ya dhuluma za wakati wa kombe la dunia
31/03/2026 Duración: 10minRipoti ya shirika la Amnesty Interenational imeonya kuwa Kombe la Dunia la mwaka huu linaweza kuchangia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dunaini kutokana mpango wa mataifa wenyeji kuweka mikakati kali za uhamiaji na ufuatiliaji wa karibu wa mashabiki wa kigeni Je, unahisi mashabiki kutoka Afrika Mashariki watakuwa salama kushabikia timu zao kule Merekani,Mexico na Canada? Skiza maoni ya waskilizaji.
-
Uganda : Kuondoa magari mabovu jijini Kampla
30/03/2026 Duración: 09minKatika makala haya tunajadili hatua ya jiji la Kampala nchini Uganda kutatangaza makataa ya siku 20 kwa wamiliki wa magari ya usafiri wa uma kuondoa magari yaliyochakaa barabarani, mamlaka zikisema lengo ni kupunguza ajali na uchafuzi wa hali ya hewa mjini. Tunakuuliza, nchi nyingine za Afrika mashariki zinapaswa kuiga mpango huu? Skiza maoni ya waskilizaji hapa.
-
Kila Ijumaa RFI kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote ile
27/03/2026 Duración: 10minMashabiki wa rfi Kiswahili kila Ijumaa hupata nafasi ya kuchangia mada yoyote ile kupitia makala haya. Skiza maoni ya baadhi ya waskilizaji.
-
Kufungwa kwa makanisa nchini Rwanda ni kwa lengo la uwajibikaji
26/03/2026 Duración: 09minRais wa Rwanda Paul Kagame amekanusha madai kuwa serikali yake imekuwa ikiminya uhuru wa kuabudu, akisisitiza kwamba hatua ya serikali kufuatilia taasisi za kidini ni kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji, na kuwalinda raia dhidi ya ulaghai,
-
Jez ni sahihi kwa wanasiasa kutusiana kwenye mikutano ya hadhara?
24/03/2026 Duración: 10minNchini Kenya, rais William Ruto na aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua, wamekuwa wakirushiana maneno makali, kwenye mikutano ya hadhara na hata kwenda mbali na kutoa matusi na kushambuliana kuhusu maumbile yao, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Nini mtazamo wako kuhusu kauli za viongozi hawa ? Katika nchi yako wanasiasa, wanatupiana maneno hivi ?
-
CAF iliivua Senegal ubingwa na kuipa Morocco baada ya miezi miwili
20/03/2026 Duración: 09minKatika uamuzi wa kushangaza , Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limefuta ushindi wa Senegal kama mabingwa wa taji la AFCON na kulipa taji hilo Morocco ambao walikuwa wenyeji wa michuano hiyo.
-
Mahakama ya kikatiba ya Uganda yafuta vipengee vilivyominya uhuru wa kusema
20/03/2026 Duración: 09min -
Urusi imehakikishia Kenya haitawasajili raia wake kupigana vita vya Ukraine
20/03/2026 Duración: 09minNchi zaidi za Afrika zimejitokeza kusema raia wake walihadhaiwa na kusajiliwa kwenda kupigana na vikosi vya Urusi nchini Ukraine
-
Bobi Wine ameweka hadharani alikimbia nchi yake baada ya kuhangaishwa
20/03/2026 Duración: 10minKiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Uganda Bobi Wine baada ya kuwa mafichoni kwa miezi miwili alifunguka na kusema kafanikiwa kukimbia baada ya kuwindwa na vikosi vya usalama
-
DRC : Mapendekezo ya kurekebisha katiba yaibua hisia mseto
12/03/2026 Duración: 10minTunajadili kinachoendelea nchini DRC, ambapo mjadala kuhusu mapendekezo ya kufanyia katiba marekebisho, ikiwemo muhula wa urais, unazidi kuibua hisia mseto, baadhi ya raia wakionekana kuunga mkono na baadhi kupinga. Unazungumziaje mjadala huu nchini DRC? Skiza maoni ya mskilizaji.
-
EAC : Kenya na Rwanda yakumbatia camera za siri barabarani
11/03/2026 Duración: 09minTunajadili hatua ya Mataifa ya Kenya na Rwanda, kuanza kukumbatia matumizi ya kamera za siri barabarani ili kunasa madereva wanaokiuka sheria za barabarani, hatua inayolenga kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikisababisha vifo maelfu ya raia. Je, unafikiri kamera za siri barabarani zitasaidia kupunguza ajali za barabarani? Ndilo swali tumekuuliza. Skiza maoni ya baadhi ya waskizaji.