Habari Rfi-ki

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:59:50
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episodios

  • Waasi wa M23 huko DRC wajiimarisha katika kutengeneza serikali mbadala

    07/10/2025 Duración: 10min

    Waasi huko mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wameendelea kujiimarisha kiutawala, kisiasa na kimiundo mbinu katika kujenga barabara, kutangaza orodha ya mawakili, hatua inayodhihirisha kuwa waasi hao wanaendea kutengeneza serikali mbadala na ile ya Kinshasa. Makala ya habari rafiki inaangazia hatua hiyo 

  • Rais mstaafu wa DRC Joseph Kabila ahukumiwa kifo, maoni ya wasikilizaji

    01/10/2025 Duración: 10min

    Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC imemhukumu rais mstaafu wa nchi hiyo Joseph Kabila Kabange adhabu ya kifo bila ya yeye mwenyewe kuwepo mahakamani, ikimtia hatiani kwa usaliti na uhalifu dhidi ya binadamu. Chama chake PPRD kimesema kesi hiyo ni ya kisiasa dhidi ya mpinzani mkubwa wa serikali. Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anaungana na wasikilizaji wa Idhaa kupata maoni yao kuhusu kesi hii, makinika kwa kusikiliza makala hii.-

  • Serikali ya DRC kusitisha leseni za makanisa na taasisi za kisheria

    30/09/2025 Duración: 10min

    Serikali ya DRC kupitia wizara ya sheria imesitisha utoaji wa leseni za Makanisa, katika kupambana na Rushwa! kwa maoni yako unaamini kusitisha utoaji wa leseni kutasaidia kupambana na rushwa? Hali ya rushwa ikoje katika taasisi za umma nchini mwako? Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka pamoja na wasikilizaji wetu wanajaribu kupata jibu kwa maswali hayo

  • Tume ya uchaguzi nchini Kenya yazindua zoezi la uandikishaji wapiga kura

    30/09/2025 Duración: 10min

    Makala ya habari rafiki ya jumatatu septemba 29 2025 imeangazia hatua ya tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC kuzindua zoezi la kuwaandika wapiga kura ambalo limeonekana kuwavutia vijana wengi, maarufu kama Gen Z.Tumekuuliza msikilizaji je? unaona vijana wote wako tayari kujiandikisha na katika nchi yako vijana wanahamasishwa vipi. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka, kwa kutuma maoni ya sauti kupitia nambari yetu ya whatsApp: +254110000420 ama pia kupitia Facebook : RFI Kiswahili  

página 2 de 2