Sinopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodios
-
Maandamano nchini Kenya kupinga mswada wa fedha 2024, hali ya usalama DRC
22/06/2024 Duración: 20minMakala imeangazia hatua ya wabunge wa Kenya kuidhinisha mswada wa fedha wa 2024 kuingia katika hatua ya pili kabla ya kupitishwa licha ya maandamano makubwa nchini, ziara ya rais Felix Tshisekedi huko Lubumbashi, na kuendelea kwa mapigano kati ya FARDC na waasi wa M23, Uganda yawasamehe waasi wa zamani wa ADF, kuapishwa kwa rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa, hali huko Afrika Magharibi, na kwengineko duniani
-
Nchi za Afrika mashariki zawasilisha bajeti, serikali mpya DRC yazinduliwa
15/06/2024 Duración: 20minTunayoangazia ni pamoja na kutangazwa kwa badgeti ya mwaka 2024/2024 kwenye nchi za jumuia ya Afrika mashariki, serikali ya mwanamke wa kwanza aliyeteuliwa kuwa waziri mkuu mpya huko DRC ilizinduliwa wiki hii, mauaji ya ADF huko Lubero mashariki mwa nchi hiyo, kifo cha makamu rais wa Malawi katika ajali ya ndege, lakini tutaangazia yaliyojiri Afrika Magharibi, kabla ya kuelekea kwengineko duniani
-
Mapigano Kanyabayonga DRC, katibu mkuu mpya wa EAC, na mengineyo
08/06/2024 Duración: 20minMakala hii imeangazia mkutano wa viongozi wa afrika huko Korea Kusini, hali ya wasiwasi kutanda kwenye mji wa Kanyabayonga, na mashirika kadhaa ya misaada kuanza kuhama, Burundi na kampeni ya kuvunja ndoa zisizorasmi, hotuba ya rais wa Uganda Yoweri M7, siasa za nchini Kenya, juhudi za kimataifa kuhusu amani ya Sudan, hali ya kisiasa Afrika kusini baada ya uchaguzi, hali ya usalama huko Gaza na siasa za Marekani
-
Serikali yatangazwa DRC, ndege aliyokodisha rais Ruto yazua gumzo na mengineyo
01/06/2024 Duración: 20minTunayoangazia wiki hii ni pamoja na uteuzi wa baraza jipya la mawaziri huko DRC pia kuendelea mapigano eneo la mashariki mwa nchi hiyo, mchakato wa uchaguzi wa mwezi Julai nchini Rwanda, safari ya rais wa Kenya William Ruto huko Marekani na ndege aliyotumia ilivyozua gumzo, juhudi za kimataifa kuhusu amani ya Sudan, uchaguzi wa Afrika kusini, Hali ya Gaza na siasa za Marekani.