Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Rais Ruto aibua hisia kali kwa kuwaagiza polisi kuwapiga risasi ya miguu waandamanaji

Informações:

Sinopsis

Wiki hii watu wasiopungua 38 waliuawa nchini Kenya kufuatia maandamano ya SabasAba siku ya Jumatatu. Rais Ruto aliibua hisia kali alipowaagiza polisi kuwapiga risasi ya miguu waandamanaji. Lakini pia, malalamiko yaliwasilishwa rasmi huko Brussels, dhidi ya wanafamilia tisa wa rais wa DRC Félix Tshisekedi, ambao wana uraia wa Ubelgiji, wakituhumiwa kwa wizi wa madini ya nchi yao. Tutakujuza pia taarifa za kikao cha Rais wa Marekani Donald Trump na marais sita wa Afrika magharibi kilichofanyika, lakini pia Uingereza na Ufaransa kutangaza rasmi mpango wa majaribio wa kuwarudisha Paris baadhi ya wahamiaji wanaowasili nchini humo kwa kutumia boti ndogo.