Sinopsis
Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzungusha dunia nzima kupitia mawimbi ya RFI Kiswahili.
Episodios
-
Rais wa DRC Felix Tshisekedi athibitisha kuwa uchaguzi utafanyika mwaka 2023
29/09/2021 Duración: 10minRais wa DR Congo Felix Tshisekedi amewaambia viongozi wa dunia kuwa uchaguzi mkuu utafanyika nchini mwake mwaka 2023 kama ilivyopangwa kikatiba.Kauli hii pia imeungwa mkono na spika wa Bunge la kitaifa huko DRC Chistophe Mboso Nkodia wakati wa Mkutano wake na Raia kwenye mji wa Kinshasa Siku ya Jumapili iliyopita.Hata hivyo Tume ya Uchaguzi inayotakiwa kuandaa uchaguzi huo, haijawekwa wazi.
-
Joto la kisiasa kuelekea uchaguzi nchini Kenya 2022
15/09/2021 Duración: 10minMakala haya mJadala wa wiki tunajadili siasa za Kenya kuelekea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa rais wa hapo mwakani.
-
Mapinduzi nchini Guinea na hali ya kisiasa kwa watawala barani Afrika
10/09/2021 Duración: 10minKwenye Mjadala wa wiki, tunaangazia hali ya kisiasa nchini Guinea na nini sababu za kutokea mapinduzi ya serikali barani Afrika. Swala ni kwa nini imejengeka dhana kwamba kiongozi anayeng'ang'ania madaraka mwisho wake siku zote ni mapinduzi ya kijeshi, nini kifanyike ili ifike mahali demokrasia na watawala waheshimu katiba za nchi zao?Mjadala wa wiki na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
-
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amtaka naibu wake ajiuzulu
25/08/2021 Duración: 13minKwenye Mjadala wa wiki, tunaangazia hali ya kisiasa nchini Kenya. Wiki hii, rais Uhuru Kenyatta amemwambia naibu wake William Ruto ajiuzulu iwapo anaona hafurahishwi na ajenda ya serikali ambayo yeye ni mdau mkubwa.
-
Siku 100 za Waziri Mkuu wa DRC Sama Lukonde
12/08/2021 Duración: 09minTunajadili siku 100 za serikali ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Sama Lukonde.
-
Siasa za vyama nchini Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu
15/07/2021 Duración: 10minKenya inajiandaa kuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2022. Vyama vya siasa vimeanza maandalizi kujiweka tayari kwa uchaguzi huo. Lakini je, vyama hivi vimejiandaa vya kutosha ? Tunajadili.
-
Miaka minne ya rais wa Tanzania John Magufuli
06/11/2019 Duración: 15minRais wa Tanzania John Magufuli, ametimiza miaka minne madarakani, je ni mafaniko gani na changamoto zipi zilizoshuhudiwa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ?
-
Hatima ya Uchaguzi Mkuu nchini Msumbiji
16/10/2019 Duración: 12minWananchi wa Msumbiji, wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu baada ya kupiga kura siku ya Jumanne. Ni uchaguzi ambao wachambuzi wa siasa wanasema ni kipimo cha demokrasia na utekelezwaji wa mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya waasi wa Renamo na serikali, miezi miwili iliyopita. Tunajadili suala hili.
-
Dunia kuangazia mabadiliko ya tabia nchi
25/09/2019 Duración: 11minMabadiliko ya tabia nchi yamechangia kuyeyuka kwa theluji katika milima mbalimbali Duniani hatua inayoisukuma nchi ya Ufaransa kuja na mradi wa kufanya utafiti ili kuhifadhi barafu unaoitwa Kumbukumbu ya Barafu iliyopo katika Mlima mrefu barani Afrika wa Kilimanjaro.Hayo yanajiri wakati huu dunia ikiangazia namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
-
Rais wa DRC Felix Tshisekedi azuru Ubelgiji kuimarisha uhusiano
18/09/2019 Duración: 13minRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi,yupo ziarani nchini Ubelgiji. Ni ziara yake ya kwanza barani Ulaya, baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa DRC mapema mwaka huu. Tshisekedi yupo nchini Ubelgji, kuhimiza ushirikano kati ya nchi hizo mbili, uhusiano ambao ulikuwa baridi wakati wa uongozi wa rais wa zamani Joseph Kabila.Je, ziara hii ina umuhimu gani kwa raia wa DRC na kwanini inazua maswalimengi maswali miongoni mwa raia wa DRC wauishio nje na ndnai ya nchi ? Kujadiki hili, tunauganba na Raphae Bakema, mchambuzi wa siasa za DRC naeneo la Maziwa Makuu, akiwa Goma lakini Profesa Malonga Pacique akiwajijini Kgali.
-
Baraza huru laundwa nchini Sudan
21/08/2019 Duración: 15minBaraza huru kati ya viongozi wa kijeshi na kiraia limeundwa nchini Sudan, kuongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka mitatu, je, litatimiza mahitaji ya raia wa Sudan ? Tunajadili.
-
Mkutano wa 39 SADC kuangazia uchumi wa viwanda
07/08/2019 Duración: 15minKaribu katika makala ya mjadala wa wiki.Kikao cha 39 cha viongozi wa mataifa ya SADC kinataraji kuanza jijini Dar es salaam nchini Tanzania ajenda kuu ni kujadili mkakati wa kiuchumi kwa kuhimiza viwanda katika mataifa hayo.Fuatilia kwa kina,wachambuzi Wetengere Kitojo na Saidi Msonga wameangazia kinaga ubaga katika makala haya na mwandishi wetu Martha Saranga.
-
Nani atamaliza Ebola nchini DRC ?
24/07/2019 Duración: 15minWiki hii Waziri wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Oly Ilunga alitangaza kujiuzulu, baada ya kushtumu uamuzi wa rais Felix Tshekedi kumwondoa kwenye Kamati maalum ya kupambana na janga la ugonjwa hatari wa Ebola, ambao tangu mwezi Agosti mwaka 2018, umesababisha vifio vya watu 1,700 na wengine zaidi ya 200 kuambukizwa katika jimbo la Kivu Kaskazini. Nani atasaidia kumaliza Ebola nchini DRC na juhudi za WHO zinafua dafu ?
-
Mauaji nchini Ethiopia yanalenga kuharibu mipango ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ?
26/06/2019 Duración: 12minMnadhimu Mkuu wa jeshi nchini Ethiopia Jenerali Seare Mekonnen ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake jijini Addis Ababa, sawa na rais wa jimbo la Amharic Ambachew Mekonen ambaye alishambuliwa na watu wenye silaha. Ni mauaji yanayokuja wakati huu, Waziri Mkuu Abiy Ahmed akiendeleza mageuzi nchini mwake. Hii inamaanisha nini ? Tunachambua na wachambuzi wa siasa za Kimataifa Haji Kaburu, Comrad Sambala wote wakiwa jijini Dar es salaam nchini Tanzania. Emmanuel Makundi, anashiriki pia, ni Mwanhabari wa RFI Kiswahili.
-
Machafuko nchini Sudan, maafa na majeruhi yaripotiwa
05/06/2019 Duración: 14minWiki hii, uongozi wa kijeshi nchini Sudan, uliamua kuvunja kambi ya waandamanaji jijini Khartoum ambao wamekuwa wakishinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.Watu zaidi ya 60 walipoteza maisha na mamia kujeruhiwa. Nini hatima ya Sudan ? Tunajadili.
-
DRC yampata Waziri Mkuu baada ya kusubiri miezi mitano
23/05/2019 Duración: 12minHatimaye rais wa DRC Felix Tshisekedi amemteua Sylvestre Ilunga kuwa Waziri Mkuu. Hii inakuja baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya rais huyo na mwenzake wa zamani Joseph Kabila. Matarajio ya raia wa DRC ni nini ?
-
Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu ataka maandamano dhidi ya rais Tshisekedi
02/05/2019 Duración: 15minKiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu, anataka maandamano yafanyike nchini humo kumshinikiza rais Felix Thisekedi aondoke madarakani kama ilivyokuwa nchini Sudan na Algeria.Fayulu anasema yeye ndiye aliyeshinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018.Tunachambua hili kwa kina.
-
Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu
03/04/2019 Duración: 12minBaada ya kuwa madarakani kwa miaka 20 hatimaye Abdulaziz Bouteflika amelazimika kusalimu amri na kujiuzulu kama rais wa nchi wa Algeria.Nini hatima ya nchi ya Algeria baada ya kujiuzulu kwa Bouteflika mwenye umri wa miaka 82 ambaye tangu mwaka 2013 amekuwa akitumia gari la magurumu baada ya kupatwa na kiharusi.Kwa mujibu wa Katiba, Spika wa Senate sasa ndio rais wa muda hadi pale Uchaguzi mpya utakapofanyika.
-
IS ladhoofishwa Syria na Iraq
27/03/2019 Duración: 12minBaada ya miezi ya mapigano, kikundi cha jihadi cha Kiislam (IS) kimepoteza Baghuz, kijiji cha mashariki mwa Siria ambacho kinaelezwa kuhitimisha utawala wa kihalifa nchini syria.Kama ambavyo mwishoni mwa 2017, IS ilivyopoteza ngome zake za Mosul nchini Iraq na Raqqa nchini Syria.
-
Mvutano kati ya Rwanda na Uganda Marekani yatia neno
13/03/2019 Duración: 12minMakala ya mjadala inaangazia mvutano wa kidiplomasi akati yamataifa mawili ya Afrika mashariki,Uganda na Rwanda wakati huu jumuiya ya Afrika mashariki ikiwa kimya..wachambuzi Abbas Mwalimu na Haji Kaburu wanadadavua kwa kina.