Habari Za Un

30 MEI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya elimu kwa watoto mashariki mwa DRC na Mkutano wa pili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT unaofunga pazia leo jijini Nairobi Kenya. Makala inaturejesha nchini DRC na mashinani inatupeleka katika bonde la Ziwa Victoria, kulikoni?Wakati ghasia zinazoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinaripotiwa kusababisha zaidi ya watoto milioni 1.8 kutokuweko shuleni, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini humo linajitahidi kwa udi na uvumba kuhakikisha watoto wanapata elimu kwani ni haki yao ya msingi.Mkutano wa pili wa siku mbili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT leo unafunga pazia jijini Nairobi Kenya. Baraza hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne ni chombo cha juu kabisa duniani cha kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya miji endelevu na limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau m