Habari Za Un

Walinda amani kutoka Tanzania TANZBATT 11 wajivunia kazi zao za kuwaunga mkono raia DRC

Informações:

Sinopsis

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC jimboni Kivu Kaskazini katika kitongoji cha Mavivi tunakutana na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 11, TANZBATT11, wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wakielezea sio tu majukumu yao, bali pia wanajivunia kile wanachofanya kwa kuzingatia Mei 29 imeadhimishwa siku ya kimataifa ya walinda amani. Afisa Habari wa TANZBATT 11 Meja Fadhila Nayopa amefuatilia hadithi zao.