Habari Za Un

Kuelekea Mkutano wa Bahari UNOC3, UNEP yatoa wito wa hatua za kukabili taka za plastiki

Informações:

Sinopsis

Katika kuelekea Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari UNOC3, utakaofanyika mjini Nice, Ufaransa kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025, Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa bahari, hasa wa taka za plastiki. Akizungumza na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNIC jijini Dar es Salaam, Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, alisisitiza umuhimu wa kushughulikia kwa haraka tatizo la taka za plastiki ambazo nyingi hutokea nchi kavu na kuishia baharini.