Habari Za Un

04 JUNI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunaangazia haki za jamii za Ogiek nchini Kenya, na masuala ya baharí na tabianchi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Mtaalamu wa UN ataka kusitishwa mara moja kwa uwekaji  mipaka unaotishia haki za Waogiek Kenya. Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaka Serikali ya Kenya kusitisha mara moja shughuli za uwekaji mipaka katika Msitu wa Mau Mashariki nchini humo, akisema kuwa unakiuka haki za jamii ya asili ya Waogiek na kupuuza maamuzi ya lazima ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR).Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki. Akiwa huko Hamburg nimemuuliza Madina ni kipi amejulisha washiriki wenzake kuwa kinapaswa kufanyika ili dunia iwe endelevu?.Makala, katika