Habari Za Un

23 MEI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunaangazia haki za kibinadamu za raia nchini Uganda, na simulizi ya mkimbizi nchini Mexico ambaye alikimbia machafuko nchini mwake Haiti. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Ethiopia, kulikoni?Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa , Volker Türk, leo Ijumaa mjini Geneva, Uswisi kupitia msemaji wake ameelezea wasiwasi wake kuhusu kupitishwa kwa muswada uliopendekezwa na Bunge la Uganda unaoruhusu raia kuhukumiwa katika mahakama za kijeshi.Wakati raia wa Haiti Giovanni Rotschild alipowasili Mexico mwaka 2022 baada ya safari ndefu isiyo na uhakika kutoka nchi mwake kulikosheheni ghasia, hakufahamu mtu yeyote wala hakuzungumza kabisa lugha ya kispanyola. Lakinialipata msaada kumwezesha kujenga upya maisha na kupata jamii mpya.Makala tukielekea siku ya kandanda, kabumbu au mpira wa miguu duniani itakayoadhimishwa Jumapili wiki hii Mei 25 ikibeba maudhui nguvu ya kdandanda katika kuleta mabadiliko tuabisha hodi Nairobi Kenya ambapo leo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Gl