Habari Za Un

27 MEI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kuangazia siku ya familia iliyokutanisha wadau wakimulika pamoja na mambo mengine nafasi ya vyombo vya habari katika kuimarisha malezi na makuzi ya mtoto.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura OCHA hii leo imesema wakati mpango tata wa Israeli wa kugawa misaada kwenye eneo la Palestina la Gaza linalokaliwa kimabavu na Israeli ukiendelea, Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena umesihi mamlaka za Israeli kuruhusu ongezeko la kiwango cha misaada ya kufikia walengwa kwenye eneo hilo lililozingirwa ili kuepusha uhaba wa chakula..Kadiri nchi zinavyokumbwa zaidi na majanga ya asili, gharama halisi za majanga ni mara 10 zaidi ya ilivyodhaniwa hapo awali, zikiwa na athari mbaya zaidi katika sekta za afya, makazi, elimu na ajira, imesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari za majanga katika ripoti iliyochapishwa Jumanne.Nchini Namibia, makazi yaliyojengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi