Habari Za Un

29 MEI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa ikitupeleka nchini DRC, Sierra Leone na Ghana. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na maana ya neno "MISHEMISHE.”Leo ni Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani ambayo mwaka huu inajikita na maudhui ya “mustakabali wa ulinzi wa amani.”Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema walinda amani wa Umoja wa Matafa wako katika changamoto kubwa “Leo hii, walinda amani wanakabiliwa na hali zinazozidi kuwa ngumu katika dunia inayozidi kuwa na changamoto, ikiwemo uugawanyika na kutofautiana kwa mitazamo duniani kunazidi kuongezeka, operesheni za ulinzi wa amani zinakabiliwa, hatari zaidi kutokana na wingi wa vitisho kama vile ugaidi na walinda amani kulengwa kwa makusudi kupitia taarifa potofu zenye madhara makubwa na changamoto zinazovuka mipaka kuanzia janga la mabadiliko ya tabianchi hadi uhalifu wa kimataifa.Kikosi cha 11 cha Tanzania kinachohudumu chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchi