Habari Za Un
WHO: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanachangia nusu ya vifo chini ya umri wa miaka 70
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:02:14
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya takwimu za afya duniani iliyochapishwa jana Mei 15 ikionesha athari kubwa zaidi za kiafya zilizosababishwa na janga la COVID-19 kuhusu vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla, imeweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili pekee, kati ya mwaka 2019 na 2021, matarajio ya kuishi yalipungua kwa mwaka mmoja na miezi nane ikiwa ni maporomoko makubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni hali iliyobatilisha mafanikio ya afya yaliyopatikana kwa muongo mmoja.