Habari Za Un
16 MEI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:12:25
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula, na takwimu za afya za janga la COVID-19 kusababisha vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini DRC, kulikoni?Ukosefu wa uhakika wa kupata chakula na utapiamlo kwa watoto uliongezeka kwa mwaka wa sita mfululizo mwaka 2024, na kuwatumbukiza mamilioni ya watu karibu na baa la njaa, huku wengine wakiepuka kutokana na misaada ya kimkakati. Imesema Ripoti ya Kimataifa kuhusu Janga la Chakula (GRFC) iliyotolewa leo huko Roma, Italia na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO.Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya takwimu za afya duniani iliyochapishwa jana Mei 15 ikionesha athari kubwa zaidi za kiafya zilizosababishwa na janga la COVID-19 kuhusu vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla, imeweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili pekee, kati ya mwaka 2019 na 2021, matarajio ya kuishi yalipungua kwa mwaka mmoja na miezi nane ikiwa ni