Habari Za Un
21 MEI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:59
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mradi wa kutengeneza barabara katika kaunti ya Meru nchini Kenya. Makala tunaangazia simulizi ya mkurugenzi na mwanzilishi wa filamu iitwayo FURU, na mashinani tunakwenda Tanzania.Wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa leo wamesema kwamba bado wanangoja kibali kutoka kwa Israel ili kusambaza msaada wa kuokoa maisha ulioruhusiwa kuingia Gaza mwanzoni mwa wiki ambapo malori matano yalifanikiwa kuingia baada ya vikwazo kwa wiki 11.Nchini Kenya, katika kaunti ya Meru hatua rahisi iliyochukuliwa inaleta mabadiliko makubwa na dhahiri kwani maeneo ambako awali barabara zilikuwa hazipitiki na hakuna mawasiliano, ubunifu wa kijapani umerejesha matumaini.Katika makala wakati ulimwengu ukiendelea kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, tunaelekea nchini Mali, ambako Fatou Cissé, mkurugenzi wa filamu na mwanzilishi wa filamu iitwayo FURU, anatumia sanaa kuangazia suala zito la ndoa za kulazimishwa.Na mashinani, fursa ni y