Habari Za Un

22 MEI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini kumsikia mgeni wetu Prof. Wallah Bin Wallah, mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Kiswahili kutoka Kenya ambaye anamulika umuhimu wa vitabu katika kukuza lugha ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari, msaada wa kuokoa maisha umefika Gaza. Baada ya wiki 11 za kizuizi kutoka kwa mamlaka za Israeli, malori 198 yaliyobeba chakula, dawa na unga wa ngano yameingia leo kupitia mpaka wa Kerem Shalom kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Mratibu mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, ameiitaja hatua hiyo kuwa ya muhimu sana, huku malori 90 yakipakuliwa usiku kwa ajili ya kusambazwa haraka.Mwaka 2024, vita havikuishia kwenye uwanja wa mapambano pekee      vilivunja nyumba, masoko na shule. Kuanzia Gaza hadi Ukraine, Sudan hadi Myanmar na zaidi ya raia 36,000 walipoteza maisha yao katika mizozo 14 ya kivita kulimgana na ripoti ya Katibu Mk