Habari Za Un

13 MEI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika lengo namba moja la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG1 la kutokomeza umaskini na inatupeleka nchini Tanzania ambako Umoja wa Mataifa umeona bora kusaidia wafugaji kuku kuondokana na umaskini.Katika mkutano wa ngazi ya mawaziri kuhusu mustakabali wa ulinzi wa amani unaofanyika leo mjini  Berlin Ujerumani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza vipaumbele vitatu vya msingi katika mageuzi ya ulinzi wa amani kwa muktadha wa dunia inayobadilika kwa kasi.Mashariki ya Kati leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeonya kuhusu vifo vya watoto kutokana na utapiamlo Gaza, sababu kubwa ikiwa ni kuendelea kukosekana kwa msaada wa kibinadamu unaojumuisha lishe maalum kwa watoto.Wakati mahitaji ya kibinadamu yakizidi kuongezeka duniani watu milioni 308 katika nchi 73 wakihitaji msaada wa dharura , Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women limeonya kuwa wanawake na wasichana ndio wanaoathirika zaidi wa migogoro, wakik