Habari Za Un
14 MEI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:10:48
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia haki za wanawake na wasichana nchini Sudan na hali ya kina mama na wanawake wajawazitio katika ukanda wa Gaza. Makala tukwenda nchini Burundi na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Wataalamu huru wa haki za binadamu, leo Mei 14 wamekemea vikali ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan ukiwemo ukatili wa kingono unaohusiana na vita, utekaji nyara, na mauaji, ambayo mengi yameripotiwa kufanywa na kundi la kijeshi la Rapid Support Forces (RSF).Huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, wanawake na wasichana wakiwemo wanawake wajawazito na wale waliojifungua, wamelazimika kukimbia makazi yao na wanaishi katika mazingira hatarishi bila huduma za msingi za kiafya. Sharon Jebichii anaangazia simulizi ya mama mmoja, mkazi wa kambi ya wakimbizi ya Jabalia, Kaskazini mwa Gaza, ambaye alijifungua akiwa amekimbia vita,na sasa anahangaika kumtunza binti yake mchanga.Katika makala Assumpta Massoi kwa makala hiyo na zaidi ya yote shirika la Umoja wa M