Jua Haki Zako

Kenya : Sanaa ya wanafunzi wa shule yakera serikali

Informações:

Sinopsis

Mjadala makali bado unaendelea baada ya serikali kudaiwa kuzuia wanafunzi wa shule ya upili ya Butere kuwasilisha uchezo wao wa Echoas of War kwenye ngazi ya kitaifa kwenye mashindao ya kuingiza. Kisa na maana ni kwamba mchezo huo unaikosoa serikali na kwamba uliandikwa na mwanasiasa ambaye ni katibu mkuu wa zamani wa chama tawala cha UDA, Bwana Cleophas Malala. Kauli ya wanafunzi kupitia mchezo wa kuigiza wa "Echoes of Doom" imeibua maswali mazito kuhusu uhuru wa kujieleza, demokrasia na usalama wa taifa.Wanafunzi hawa walitumia jukwaa la sanaa kuelezea hali  halisi ya jamii, lakini kile kilichoanza kama onyesho la kisanaa , limeibua hisia mseto baada ya madai kwamba serikali iliwazuia wanafunzi hao kuonyesha sana hiyo kwenye ngazi ya kitaifa. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.