Gurudumu La Uchumi

Sehemu I: Madhara ya ushuru wa Trump kwa bara la Afrika na biashara ya dunia

Informações:

Sinopsis

Kwa majuma kadhaa, mijadala mikali duniani kote kufuatia uamuzi wa rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza ushuru zaidi wa bidhaa zinazoingia kwenye taifa hilo, mataifa ya Afrika yakiwa miongoni mwa waathirika, baadhi wakiwekewa ushuru wa hadi asilimia 50. Katika makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunadadavua na wataalamu athari za ushuru wa Trump kwa nchi za Afrika na biashara ya dunia kiujumla. Tutakuwa na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.