Habari Za Un

Tutahakikisha Kiswahili kinasambaa duniani na kusongesha ajenda za UN: Dkt. Ndumbaro

Informações:

Sinopsis

Kongamano la kimataifa la Kiswahili leo limeng’oa nanga jijini Havana Cuba likiwaleta pamoja takribani washiriki 400 kutoka Afrika, Asia, Amerika na Ulaya ili kujadili ajenda mbalimbali za kupanua wigo wa luugha hiyo na kuitumia kuleta tija ikiwemo kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa kama amani na maendeleo endelevu. Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Kongamano hilo Waziri wa utamaduni, sanaa na michezo wa Tanzania Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amesema hili ni kongamano la kimataifa la Kiswahili na ajenda yake kuu ni kukifanya Kiswahili kivuke mipaka.