Habari Za Un

UNICEF na wadau Somalia wafanikisha mradi wa maji kwa wakazi wa Galmudug

Informações:

Sinopsis

Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika. Tuko Adale, mji wa ndani zaidi wa jimbo la kati mwa Somalia, Galmudug. Hapa zaidi ya kaya 2,000 sasa zina huduma ya maji safi na salama, kufuatia ukarabati wa kisima cha maji.Salada Mohammed Omar, yeye ni mfugaji na ni shuhuda wa mradi huu uliotekelezwa na serikali ya jimbo la Galmudug kwa ufadhili wa shirika la Marekani la Misaada ya kimaendeleo USAID na UNICEF.“Tulisafiri muda mrefu kuteka maji, lakini sasa kisima kiko karibu na makazi yetu, tunapata kwa urahisi maji ya kupikia, kufulia na kufanyia usafi.”Video ya UNICEF inaonesha raia na ngamia wakiwa kisimani. Mohammed Yusuf Dirshe ambaye ni kiongozi wa kijamii hapa Adale anasema “awali hakukuwa na tanki la maji wala pampu. Kwa hiyo ilikuwa vigumu kupata