Habari Za Un

UN: Baada ya janga la njaa, sasa kipindupindu na homa ya kidingapopo yaikumba Sudan

Informações:

Sinopsis

Nchini Sudan ambako vita na njanga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia  sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa  la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani. Asante Assumpta kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA na lile la afya duniani WHO, hali inazidi kuwa mbaya Sudan ambako katikati ya vita majanga mingine ya kiafya yanazuka.OCHA imeripoti zaidi ya wagonjwa 28,000 wa kipindupindu na vifo vimefikia 836 katika majimbo 11 kati ya 22 Julai na 28 Oktoba mwaka huu huku likihofia kwamba idadi kamili ya wagonjwa huenda ni kubwa zaidi.Pia shirika hilo limeonya juu ya kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa homa ya kidingapopo na mvua zinazonyesha na kusababisha mafuriko makubwa zimeongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa hayo.Nalo shirika la WHO linasema milipuko hii imezuka