Habari Za Un

Walinda amani wa UNIFIL nchini Lebanon wasimilia kinachowakabili mashambulizi ya Israel yakiendelea

Informações:

Sinopsis

Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambapo, katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya Lebanon na Israel, walinda amani walioko katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura wamekuwa wakivumilia mazingira magumu. Ushuhuda wa hivi karibuni kutoka kwa walinda amani hao unaonesha ukubwa wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo vitisho vilivyoongezeka kutoka kwa shughuli za kijeshi za Israel zilizo karibu na eneo hilo, vizuizi vya kusafiri, na changamoto za uendeshaji wa shughuli. Kupitia video ya  Kikosi hicho cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, tunaona picha ya makao makuu yake huko Naqoura, Lebanon. Hapa tunaona ofisi za walinda amani hao, karibu na ofisi hii kuna mnara wa ulinzi, sehemu yake ikiwa imeharibiwa na mlipuko. Meja Kalpani Fernando anaelekeza kwenye mnara huo akieleza kilichotokea.“Ghafla, tuliona, na kusikia mlipuko. Kisha tukaona vumbi kubwa likitokea na moshi mweusi. Tulikimbia ndani ya ofisi, na ndani ya sekunde chache, mlipu