Habari Za Un

UNICEF Kenya wafanikisha mapambano dhidi ya kipundupindu Lamu

Informações:

Sinopsis

Serikali ya Kaunti ya Lamu katika pwani ya kaskazini ya Kenya, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanaendesha shughuli ya kuwafikia wanajamii ili kubadilishana taarifa kuhusu jinsi watu wanaweza kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kutoa huduma za maji, vifaa vya kujisafi na usafi kwa jamii zilizoathirika. Kutoka katika video iliyoandaliwa na UNICEF.Wamekaa chini ya mti, wanawake kwa wanaume. Nyuma ni nyumba ya makuti na matumbawe, Lamu, Pwani ya Kenya. Muelimishaji wa masuala ya afya anawaeleza namna ya kuweka mazingira safi ili kupambana na kipindupindu. Mwanajuma Kahidi yamewahi kumkuta. Anaposema Cholera anamaanisha hiyo hiyo kipindupindu iliyokuwa imetishia Uhai wake na familia yake.“Nilipopata maambukizi ya Kipindupindu nilihisi siko sawa kwa sababu nilikosa nguvu na nikakosa raha na nikapoteza nuru ya macho ndio nikakimbilia hospitali. Huo ugonjwa ulipitia kwenye maji na chakula. Mimi na watoto wangu tulipatwa na kipind