Habari Za Un

UN Ripoti: Uwezekano wa kifo cha Dag Hammarskjöld kuwa ni hila unaongezeka kutokana na taarifa mpya

Informações:

Sinopsis

Ripoti nyingine mpya ya tathimini ya uchunguzi wa hali na mazingira ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1961 Dag Hammarskjöld imetolewa leo ikiwa na vipengele vinne vipya vikiongeza uwezekano kwamba kifo hicho cha ajali ya ndege kilikuwa ni hila. Asante Anold kwanza ikumbukwe kuwa hii sio ripoti ya kwanza na huenda isiwe ya mwisho ya kutathimini hali na mazingira yliyochangia ajali ya ndege iliyokatili maisha ya Dag Hammarskjöld tarehe 17 Septemba 1961 akiwa njia kuelekea Congo ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cngo DRC, kujadili usitishwaji wa uhasama ila ni ripoti ya karibuni zaidiRipoti inasema mwenyekiti wa jopo la tathimini ya uchunguzi jaji mkuu wa zamani wa Tanzania Mohamed Chande Othman amepokea taarifa mpya muhimu kutoka kwa nchi wanachama ambazo zinajumuisha maeneo haya Mosi:  uingiliaji unaowezekana wa Nchi Wanachama wa mawasiliano husika.Pili: Uwezo wa wanajeshi wa Katanga, au wengine, wa kufanya shambulio linalowezekana kwenye ndege ya SE-BDY,Tatu: kuwepo