Habari Za Un
11 OKTOBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:58
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike na juhudi za Umoja wa Mataifa za kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na unaofanyika mtandaoni. Makala tunakupeleka katika ukanda wa Gaza, na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.Makala tunakupeleka Gaza ambapo mwaka m