Habari Za Un
15 OKTOBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:10:51
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani kesho ikiwa ni siku ya chakula duniani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatili juhudi za FAO za kuhakikisha haki ya chakula kwa maisha bora na mustakabali bora kwa wananchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Licha ya mashambulizi, awamu ya pili ya chanjo kwa watoto dhidi ya polio huko Gaza iliyoanza jana imeendelea leo Jumanne eneo la kati mwa Gaza na hadi sasa watoto wapatao Elfu 93 wenye umri wa chini ya miaka 10 wameshapatiwa dozi ya pili.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo linatoa wito wa msaada wa dharura kuepusha janga la kibinamu eneo la kusini mwa Afrika kutokana na ukame uliochochewa na El- Niño.Na ubia mpya wa kutokomeza watu kukosa utaifa umezinduliwa huko Geneva, Uswisi ukilenga kutokomeza hadhi hiyo inayoathiri mamilioni ya watu duniani. Zaidi ya nchi 100, mashirika ya kiraia, taasisi zinazopigia chepuo kuondokana na hadhi hiyo, wanazuoni na wadau wengine wameanzisha ubia huo ikiwa ni kuendeleza kampe