Habari Za Un
17 OKTOBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:11:14
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia juhudi za vijana hasa katika kuboresha mifumo ya elimu katika matumizi ya teknolojia ambapo Gloria Anderson, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shirika la TEDI anatufafanulia zaidi.Leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema umaskini umesalia kuwa baa la dunia ukiathiri mamia ya mamilioni ya watu duniani kote.Huko MAshariki ya Kati, awamu ya pili ya utoaji wa chanjo dhidi ya polio imekamilika eneo la kati mwa Gaza, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema watoto 181,429 wamepatiwa. Wengine 148,064 wamepatiwa matone ya vitamini A. Ingawa hivyo vituo vinane vya afya vitasalia wazi ili kuendelea kutoa chanjo kwa familia zilishindwa kufikisha watoto wao katika siku tatu za chanjoMkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti amezuri Rwanda kujionea harakati za taifa hilo k