Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Kenya: Namna mabaki ya ngozi ya samaki yanavyotumiwa kuhifadhi mazingira
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:20
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Kwa miaka mingi taka inayotoka kwa samaki na viumbe vingine kwenye ziwa, imekuwa ikichafua mazingira na kusababisha samaki wengi kukosa hewa ya oxigeni hivyo kufariki na kusababisha hasara kubwa.Hata hivyo wenyeji sasa wengi wao vijana wameanza kutumia taka hizo kutengeza bayogesi na bidhaa zingine kama vile viatu,nguo,begi mifuko na kadhalika hivyo kubuni ajira na kuinua uchumi. Katika fuo za Dunga kando na ziwa Victoria kaunti ya kisumu nchini Kenya,wafanyabiashara hapa wanatumia bayogesi kukaanga samaki na kuwauzia wateja wanaotalii êneo hili.Bayogesi hii inayotengenezwa kutokana na mabaki ya samaki ,imewafaidi wenyeji wa hapa kupunguza gharama ya matumizi vile vile kutunza mazingira. Caroline Achieng ni mfanyabiashara wa samaki.“Tunadumisha usafi kwa sababu wageni wanakuja hapa lazima tudumishe usafi ndio mazingira yetu yasiharibike,mradi huo umesaidia sana kwa sababu wametusaidia kuchukuwa hizi takataka za samaki kama matumbo,wanatengeneza nayo bayogasi hivyo kupunguza uchafu”alisema Caroline Achieng m