Gurudumu La Uchumi

Changamoto na fursa kwa vijana wajasiriamali na ajira kwenye nchi za Afrika Mashariki

Informações:

Sinopsis

Hujambo msikilizaji wa rfikiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu nikukaribishe katika makala ya Gurudumu la Uchumi, na hivi leo tunaangazia ukanda wa Afrika Mashariki, eneo lililojaa nguvu kazi ya vijana pamoja na ari ya ujasiriamali, lakini bado linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira. Takwimu za hivi karibuni za benki ya dunia zinaonesha uhalisia wa tatizo, takwimu zikitofautiana baina ya nchi na nchi, lakini kiujumla ni kuanzia kati ya asilimia 4 hadi 19 ya vijana hawana ajira, huku wanawake walioko vijijini wakiwa waathirika wakubwa. Katika makala haya hivi leo, tutaangazia kwa kina namna gani bora ya kukabiliana na tatizo la ajira na kuongeza wajasiriamali wengi zaidi kwenye ukanda. Kwenye line ya simu nimewaalika, Ali Mkimo, yeye ni mchambuzi wa masuala ya Uchumi pamoja na Emmanuel Cosmas, kijana mbunifu wa masuala teknolojia na nibalozi wa UNICEF, wote hawa wakiwa nchini Tanzania.