Sinopsis
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Episodios
-
Hatuwa za mwisho za maandalizi ya tamasha la watu wa kabila la bashi la desemba 6
01/12/2024 Duración: 20minUhusiano baina ya lugha na utamaduni, mila na mirathi ya jamii kwa jumla huenda ukafahamika angalau kwa wepesi, iwapo tutazingatia mambo kadhaa ikiwemo lugha na matumizi yake, tabia, utu, utamaduni, mila,mitindo na mengineo. Watu wa kabila la washi mashariki mwa DRC wameandaa tamasha la kutambulisha utamaduni wao, ambalo ni msimu wa pili na limepangwa kufanyika desemba 6 hadi 8 huko Bukavu. Katika makala haya mtangazaji wako Ali Bilali anakuletea sehemu hii ya tatu na ya mwisho ya maandilizi ya makala haya. unaweza kusikiliza sehemu ya kwanza kubonyeza hapa (sehemu ya kwanza) Lakini pia sehemu ya pili kwa kubonyeza hapa (Sehemu ya pili) Asante kwa kuendelea kuwa muaminifu kwa radio yako na kwa mtangazaji wako asiependa makuu unaweza kumfollow kwa kubonyeza hapa Billy Bilali
-
Msani Olivier kutoka Bukavu azungumzia tamasha la watu wa kabila la washi Nov 24 2024
23/11/2024 Duración: 19minMakala haya Ali Bilali anazungumza na msanii Oliver wa nyimbo za asili ya washi wahavu mashariki mwa DRC kuelekea tamasha la Bushi ama Festival de Bushi. Asante kwa kuendelea kuwa muaminifu kwa radio yako na kwa mtangazaji wako asiependa makuu unaweza kumfollow kwa kubonyeza hapa Billy Bilali
-
Maandalizi ya Tamasha la watu wa Kabila la Washi kutoka Bukavu sehemu ya kwanza.
18/11/2024 Duración: 20min