Sinopsis
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Episodios
-
Sehemu ya Pili: Afrika na harakati za kudai mabadiliko kwenye taasisi za kifedha za kimataifa
26/02/2025 Duración: 09minMsikilizaji juma lililopita tulianza kwa kujadili yaliyotokana na mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, na suala kuu lilikuwa ni je, nchi za Afrika zitafanikiwa kushinikiza mabadiliko katika taasisi za kifedha za kimataifa na kuondokana na mikopo na madeni yasiyostahimilika ?Leo katika makala ya Gurudumu la Uchumi, nakuletea sehemu ya pili ya mjadala huu, nimemualika Ali Mkimo, mtaalamu namchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa nchini Tanzania.
-
Je, Afrika itafanikiwa kushinikiza mabadiliko katika mifumo ya kimataifa ya kifedha
19/02/2025 Duración: 10minMsikilizaji mwishoni mwa wiki iliyopita, viongozi wa Afrika waliokutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, walikubaliana kuongeza kasi ya kudai mabadiliko kwa mifmo ya kifedha ya kimataifa, ili kuziwesha kuwa na nafasi katika maamuzi. Afrika inalalamika kutokuwepo usawa, na hivyo kuyaweka mataifa ya Afrika katika hali ya kutegemea mikopo yenye masharti magumu.Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunajadili ikiwa azma hii ya viongozi wa Afrika itafanikiwa.
-
Migogoro inavyotatiza ukuaji wa uchumi, maendeleo na utawala bora Afrika
12/02/2025 Duración: 09minHujambo msikilizaji wa RFI Kiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu, makala ni Gurudumu la Uchumi na leo hii tunazungumzia kuhusu athari za kiuchumi kutokana na mizozo kwenye nchi za Afrika.Tutazungumza na Hamduni Marcel, mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania.
-
Afrika inajifunza nini baada ya Marekani kusitisha kwa muda misaada ya nje.
05/02/2025 Duración: 09minJuma hili katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili kuhusu athari za hatua ya Marekani kusitisha kwa muda utoaji wa misaada ya nje. Uamuzi huu tayari umeonekana kutishia baadhi ya sekta zilizokuwa zinasaidiwa kupitia USAID kama vile Afya na Elimu.Tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.