Sinopsis
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episodios
-
Droo ya CHAN 2024: Kenya yapangwa kundi gumu zaidi, mashindano ya Agosti 2025
18/01/2025 Duración: 23minKipindi cha leo kimeangazia pakubwa droo ya mashindano ya CHAN 2024; adhari ya kuahirishwa kwa kipute na uchambuzi wa makundi. Pia tumetupia jicho raundi ya sita hatua ya makundi mechi za klabu bingwa Afrika, fainali ya mashindano mapya ya wasichana U17, Shujaa yataja kikosi chake cha mkondo wa Perth 7s, Kipchoge akilenga taji la tano la London Marathon, Tyson Fury astaafu ndondi kwa mara ya pili pamoja na mashindano ya tenisi ya Australian Open yakiingia hatua ya robo fainali. Kulingana na droo iliyofanyika Jumatano usiku katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi nchini Kenya, Harambee Stars imepangwa katika 'kundi la kifo' ambapo itamenyana na mabingwa mara mbili Morocco (2018 na 2020) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (2009 na 2016)."Tuko kwenye kundi la kifo," Mariga alikiri, akibainisha uimara wa wapinzani wao."Hizo ni timu kubwa na inamaanisha lazima tuweke juhudi zaidi katika maandalizi."“Wapinzani wetu ni wagumu, tutashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza lakini ha
-
CHAN 2024: Uwanja wa Nyayo nchini Kenya waidhinishwa na CAF kuandaa mashindano
11/01/2025 Duración: 23minTuliyokuandalia jioni hii ni pamoja na uchambuzi wa mashindano ya Mapinduzi, tetesi za uhamisho Afrika Mashariki, raundi ya tano ya mechi za klabu bingwa Afrika, maandalizi ya CHAN 2024, uhamisho wa wachezaji ulaya na mashindano ya tenisi ya Australian Open.
-
KENYA: Kuzaliwa, kufa na "kujaribu" kufufuka kwa mchezo wa masumbwi nchini Kenya.
08/01/2025 Duración: 38minPopote pale ulipo nikukaribishe katika Makala ya jukwaa la michezo ndani ya FRI Kiswahili.Leo tumekuandalia Makala spesheli ambayo inaangazia kushuka pakubwa kwa viwango vya mchezo wa masumbwi nchini Kenya, Makala ambayo tunayapeperusha wiki kadhaa tu baada ya kukamilika kwa michezo ya Olimpiki Jijini Paris nchini Ufaransa. Kwa mara ya kwanza katika, historia ya kenya, hakuna bondia hata mmoja aliyewakilisha taifa katika michezo ya olimpiki jijini Paris. Hatua hii ilizua ngumzo kwa wadau wa mchezo huo.Lakini, Iweje mchezo uliokuwa ukisifika na kuiletea Kenya hadhi katika miaka ya nyuma imedidimia kiasi hiki? Je, ni usimamizi mbaya ama ni ukosefu wa ligi dhabiti au ni kukosa wadhamini wa kuwekeza katika mchezo hili kuiletea fahari inayostahili. Je, Kuna uhasama kati ya wadau ama wasimamizi wameingiwa na kiburi na kujisahau na kuwasahau mabondia?Mwenzangu George Ajowi amezungumza na Mabondia wa zamani, marefa, makocha, mapromota, wanahabari na vile vile wadau wengeni katika sekta hii na kuzungumza nao kuhusiana
-
Mashindano ya magari ya Dakar Rally 2025 yang'oa nanga huko Saudi Arabia
04/01/2025 Duración: 23minLeo kwenye makala ya kwanza kabisa ya Jukwaa la Michezo mwaka 2025, tumeangazia raundi ya nne hatua ya makundi mechi za Ligi ya vilabu bingwa Afrika. Mwanariadha mkenya Beatrice Chebet avunja rekodi yake ya dunia huku raia wa Eritrea mwendesha baiskeli Biniam Girmay akishinda tuzo la Afrika wakati uo huo mashindano ya magari ya Dakar Rally na Kombe la Mapinduzi yaking’oa nanga. Lakini pia tutatupia jicho tetesi za uhamisho ulaya na michuano ya tenisi ya Brisbane Open inayoendelea.