Sinopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodios
-
DRC : Haki ya wanawake kupata elimu
05/11/2024 Duración: 10minNchini DRC, kumeripotiwa upungufu wa watoto wa kike katika kupata elimu, hili likidaiwa kuchangiwa na tamaduni zilizopitwa na wakati. Katika makala haya basi Butua Balingane, mkurugezi wa chuo kikuu cha walimu cha ISP, Goma ambaye anasimulia masaibu anayopitia mtoto wa kike nchini DRC kupata elimu. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
-
Kenya : Wanawake 97 wauawa kwa kipindi cha miezi tatu
05/11/2024 Duración: 09minNchini Kenya, idara ya polisi imekiri kwamba wanawake 97 wameuawa kwa kipindi cha miezi 3, baadhi miili yao ikipatikana imenyofolewa. Ni visa ambayo vimesababisa viongozi wa ngazi ya juu akiwemo rais William Ruto, ambaye ametoa agizo wa asasi za uchunguzi nchini humo kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika visa hivyo. Kwenya makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Kenya, ambapo mtaalamu wa maswala ya jamii bi Carolina Situma anaeleza nini kimechangia mauwaji haya.
-
Kenya : Visa vya raia kutekwa yaongezeka
25/10/2024 Duración: 09minNchini Kenya, visa vya raia kutekwa na kisha baadaye kuachiliwa au kupatikana wameuawa vinazidi kuongezeka, visa kadhaa vikiendelea kugonga vichwa vya habari. Katika Makala haya George Ajowi angaazia visa hivi na jinsi mkuu wa polisi nchini Kenya alikosa kufika mahakamani kueleza walipokuwa baadhi ya wakenya waliotekwa.