Sinopsis
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episodios
-
Vita Mashariki mwa DRC vyawaathiri maelfu ya watu Masisi
15/01/2025 Duración: 10minTunaangazia kuendelea kwa vita Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kati ya jeshi la serikali FARDC wanaoshirikiana na wapiganaji wa Wazalendo dhidi ya waasi wa M 23 wanaoungwa mkono na Rwanda. Watu zaidi ya 100, 000 wameyakimbia makaazi yao katika wilaya ya Masisi tangu kuanza kwa mwaka 2025 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.Nini suluhu ya mzozo huu ?
-
Tanzania: Mbowe na Lissu wakiweka CHADEMA njia panda
08/01/2025 Duración: 10minChama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, kitawachagua vongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho, Januari tarehe 21. Kibarua kigumu kipo kwenye ushindani wa nafasi ya Mwenyekiti.Freeman Mbowe ambaye amekuwa akiongoza chama hicho kwa zaidi ya miaka 20 na Makamu wake Tundu Lissu, ni miongoni mwa watia nia waliojitosa kupambania nafasi hiyo.Wawili hao wameendelea kutupiana maneno makali, na kuzua hofu kuhusu hatima ya chama hicho baada ya uchaguzi huo. Thomas Kibwana ni mchambuzi wa siasa za Tanzania, akiwa jijini Dar es salaam, anachambua kwa kina.
-
Msumbiji yaendelea kujipata kwenye mvutano wa kisiasa
01/01/2025 Duración: 10minHeri ya mwaka mpya wa mwaka 2025. Nchi ya Msumbiji bado ipo kwenye mvutano mkali wa kisiasa, baada ya uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka 2024.Hali imeendelea kuwa mbaya baada ya Baraza la Katiba, kuthibitisha ushindi wa Daniel Chapo kutoka chama tawala FRELIMO, kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais huku kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane, akiendelea kudai aliibiwa kura.Watu zaidi ya 260 wamepoteza maisha, wengi wao wakipigwa risasi na polisi kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu.
-
Hatua ya rais wa Kenya kuwateua wandani wa mtangulizi wake yazua maswali
25/12/2024 Duración: 10minMakala ya wimbi imeangazia hatua ya rais wa Kenya, William Ruto, kuwajumuisha katika serikali yake mawaziri kadhaa waliohudumu wakati wa utawala wa mtangulizi wake Uhuru Kenyatta, na vile vile wandani wake kinara wa upinzani Raila Odinga., na hii ni licha ya yeye kuapa kutohusisha wapinzani kwenye Serikali yake; Ruben Lukumbuka anazungumza na Edwin Kegoli pia Torosterd Alenga ni wataalamu wa siasa za Kenya.