Sinopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodios
-
Sera kuhusu idadi ya watu inavyoathiri uchumi ,afya na hali ya maisha
11/06/2024 Duración: 09minMataifa ya Afrika bado yanaendelea kushuhudia kasi ya ongezeko la watu ijapokuwa chumi za Afrika hazifanyi vizuri inavyotakikana Watalaam wanaonya iwapo idadi ya watu haitodhibitiwa ,kupangiwa huenda mataifa mengi yakalemewa na idadi ya watu wanaowategemea wengineAidha kuna hatari ya sera za serikali kushindwa kukidhi mahitaji ya raia wake ,idadi inapokuwa kubwa
-
Juhudi za kuukabili ugonjwa wa Mycetoma kutumia dawa zilizofanyiwa utafiti Sudan
08/06/2024 Duración: 10minMycetoma ni mojawapo ya magonjwa yaliyopuuzwa ingawa unaendelea kuwaathiri wengi haswa watu wanaokaa maeneo kavu na jamii zilizotengwa Mycetoma hujidhihirisha kama donda ambalo haliponi bali linaendelea kukua na kuchimba sehemu athirika katika mwili
-
Mataifa ya Afrika yashinikiza mwongozo wa kukabiliana na hali ya dharura
29/05/2024 Duración: 09minMataifa wanachama wa shirika la afya duniani ,WHO yanayokongamano katika kongamano la afya ya 77 jijini Geneva yanataka kuwepo mwongozo wa afya kukabiliana na hali ya dharura baada ya janga la COVID 19 Mataifa haya yanasisitiza kuwepo usawa kwenye kuzalisha na matumizi ya sampuli za kutengeneza sampuli zinazochangiwa na nchi mbali mbaliAidha usawa kwenye ufadhili ,usambazaji wa chanjo mpya na chanjo zinazotumika wakati wa majanga Kongamano hilo pia linatazamiwa kuja na mwafaka kuhusu marekebisho kwenye sheria za afya za mwaka 2005
-
Matatizo ya afya ya akili yasipotatuliwa huwaathiri mustakabali wa watoto
22/05/2024 Duración: 10minWatoto na vijana walioshuhudia dhulma , kupata kiwewe,mara nyingi wanajikuta hawaamini katika uhusiano ,huwa waathiriwa wa dhulma za kimapenzi