Sinopsis
Kupitia vipindi vyetu tunajaribu kuwahamasisha vijana wa Afrika kuhusu elimu ya jamii. Inasaidia kuyafanya maisha yao kuwa rahisi.
Episodios
-
Elimu – Kipindi 6 – Hadithi ya Malaika
11/03/2011 Duración: 10minMalaika ndiyo kwanza amerejea kutoka katika mahafali mjini na anakwenda nyumbani kusherehekea na familia yake. Huko ndiko majaaliwa yake yatakapoamuliwa
-
Elimu – Kipindi 5 – Hadithi ya Malaika
11/03/2011 Duración: 10minHuko chuoni, Malaika anawajibika kumaliza elimu ya vitendo ili kukamilisha mwaka wa masomo. Kwa msaada wa rafiki yake Malaika amefanikiwa kupata shirika atakakofanyia mafunzo hayo. Je anafaulu mtihani wake wa mwisho?
-
Elimu – Kipindi 4 – Hadithi ya Malaika
11/03/2011 Duración: 10minMalaika anakwenda nyumbani kwa likizo yake ya kwanza. Anaitembelea shule yake ya zamani kuwahamasisha vijana kusoma na kuzuia mipango mingine ya wazazi wake kutaka aolewe. Je anaweza kuingiliana na maisha ya kijijini?
-
Elimu – Kipindi 3 –Hadithi ya Malaika
11/03/2011 Duración: 10minMalaika anajifunza kuwa kuna vitu vya kujifunza nje ya masomo. Cindy, mkaazi mwenzake anamuonyesha jinsi ya kufurahia maisha ya chuoni lakini bado anakabiliwa na changamoto ya kutojiangusha yeye mwenyewe au kijiji chake
-
Elimu – Kipindi 2 – Hadithi ya Malaika
11/03/2011 Duración: 10minKwa msaada wa kijiji chake, na mkopo binafsi, Malaika hivi sasa anaweza kulipia ada ya chuo kikuu.Mwalimu wake wa zamani anamsindikiza katika jiji kubwa kumsaidia kujisajili na kupata makazi chuoni.
-
Elimu – Kipindi 1 – Hadithi ya Malaika
11/03/2011 Duración: 10minTutajifunza zaidi kupitia hadithi ya Malaika, jinsi ya kusoma chuo kikuu. Msichana huyo wa kijijini alijitofautisha na wengine alipowashinda wavulana wote katika mtihani wake wa mwisho shuleni. Je nini mustakhbali wake?
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 10 – Afrika Kulikoni?
11/03/2011 Duración: 11minZapcom na timu yake wameibadili taswira ya kijiji chao. Katika kipindi hiki cha mwisho, timu yetu inatuaga huku ikiendelea kutafuta fursa kubwa zinazotolewa na teknolojia mpya ya mawasiliano kwa bara laf Afrika.
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 08 – Kuamua kabla kuingia Mtandaoni
11/03/2011 Duración: 11minMjomba Kiilu amekasirika na ameifukuza timu kwenye mkahawa wa intaneti. Lakini timu hiyo imefanya kosa gani?
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 09 – Ustawi wa Biashara
11/03/2011 Duración: 11minHuku fursa za teknolojia mpya ya mawasiliano zikiongezeka, inatoa mwanya wa kupanua biashara. Bonyeza hapa uungane na timu yetu.
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 07 – Virusi na wizi wa Muziki kupitia Mtandao
11/03/2011 Duración: 11minOh Hapana! Kompyuta zote kwenye mkahawa wa intaneti zimeathiriwa na virusi. Nini kimefanyika? Na watalitatua vipi tatizo hilo?
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 05 – Kujali na Kulinda Mazingira
11/03/2011 Duración: 11minHufanya nini na simu ya zamani ya mkononi? Hutengenezwa na vifaa gani? Na husababisha athari gani kwa mazingira? Timu yetu inajaribu kujibu maswali haya.
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 06 – Kituo cha huduma za Intaneti
11/03/2011 Duración: 11minZapcom na timu yake wanagundua fursa chungu tele za mawasiliano ya kisasa kila kuchao. Wanajifunza pia jinsi ya kutumia ujuzi huu mpya katika maisha yao ya kila siku – hata katika mkahawa mdogo wa mjomba Kiilu kijijini.
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 04 – Kucheza na Kulipa
11/03/2011 Duración: 11minZapcom na timu yake walionekana kupata mawazo mapya kila mara. Hata hivyo kuna shinikizo kubwa. Ukosefu wa miundombinu hausaidii hali. Je timu hii inakabiliana vipi na hali hii?
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 02 – Kufungua Mtandao
11/03/2011 Duración: 11minRafiki yetu kijana Zapcom na timu yake wanakaribia kutimiza ndoto yao. Je watafaulu?
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 03 – Kutafiti kwenye Mtandao
11/03/2011 Duración: 11minMkahawa mpya wa huduma za intaneti umefunguliwa na unafanya kazi. Lakini kuna changamoto nyingi ambazo marafiki zetu wanajifunza kukabiliana nazo huku biashara ikikua.
-
Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano – Kipindi 01 – Mkahawa wa Intaneti
11/03/2011 Duración: 11minAnayetufungulia kipindi hiki ni Zapcom, kijana chipukizi mwenye shauku kutokana na elimu mpya aliyojifunza. Ndoto yake kubwa ni kukiinua kijiji chake. Tuungane naye.
-
Historia – Kipindi 10 – Ubaguzi
09/03/2011 Duración: 11minKatika kipindi chetu cha mwisho, babu Peter anatueleza kuhusu enzi mbaya ya historia. Kupitia hadithi zake tumejifunza mengi katika mfululizo wa vipindi hivi. Kwa bahati nzuri, tunaweza kuvikamilisha kwa furaha!
-
Historia – Kipindi 08 – Ukoloni
09/03/2011 Duración: 11minSi siri kwamba eneo kubwa la Afrika lilitawaliwa na makoloni Wazungu. Lakini ilikuwaje babu Peter? Ni kitu gani walichokitaka? Na kuzigawa nchi na watawala wao kulifanyika vipi?
-
Historia – Kipindi 09 – Makundi ya kupigania uhuru
09/03/2011 Duración: 11minTangu katikati ya karne ya 20 mataifa yote ya Afrika wamejipatia uhuru. La huzuni ni kwamba baadhi yao yalilazimika kupigana vita vya umwagaji damu kujikomboa, hasa yale yaliyokuwa chini ya utawala wa Wareno. Sawa, babu?
-
Historia – Kipindi 07 – Ustaarabu wa Kiafrika na Ukoloni
09/03/2011 Duración: 11minKatika ufalme wa zamani wa Ashanti, msichana kuvunja ungo na kuwa mwanamke lilikuwa tukio kubwa, na kila mtu alialikwa kusherekea kukua kwake! Hiyo ilikuwa mpaka ngoma zilipopigwa kutangaza kuwasili kwa mzungu